magaya2525
New Member
- Jul 27, 2022
- 1
- 0
UMUHIMU UTOAJI WA ELIMU YA AFYA NA MAZINGIRA KATIKA JAMII.
Mazingira ni jumla ya vitu vinavyomzunguka mwanadamu.
Elimu ya mazingira ni namna/taratibu/njia au mafunzo yanayoelekeza njia za utunzaji wa mazingira katika jamii.
Afya ni hali uimara kimaumbile,kijamii na kiakili au ni hali ya kutokua na mawazo,jeraha/ugonjwa
UTOAJI WA ELIMU YA KUTUNZA AFYA YA MWILI
1. Usafi wa mwili- afya ya mwili hutegemea sana usafi wa mwili hususani kuoga,kusafisha meno,ukataji wa kucha kuosha mikono kabla na baada ya kula au baada ya kutoka msalani. Njia hizi zote husaidia kuimarisha afya ya mwili.
2. Usafi wa mavazi,malazi -Nguo zinapaswa ziwe safi kwa kufuliwa pia hata malazi yanastahili usafi kuepuka magonjwa yanayo sababishwa na wadudu kama chawa.
3. Matumizi sahihi ya chanjo,kinga na vyandarua - Ni njia ya kujikinga na maradhi pia kuimarisha afya katika magonjwa ambayo hupatiwa chanjo mfano UVIKO-19 na Malaria ambayo vyandarua husaidia kuepuka mbu.
4. Matumizi ya vipimo na matibabu ya magonjwa - matumizi ya vipimo kabla ya dawa na matibabu sahihi juu ya kupambana na magonjwa husika husaidia uimara wa afya ya mwana jamii.
5. Lishe,mazoezi na muda wa kupumzika-Lishe bora na mazoezi husaidia kujenga na kuimarisha afya pia muda wa kupumzika huupa mwili nguvu na uwezo wa kupambana na magonjwa .
UMUHIMU WA UTOAJI ELIMU HII KWA JAMII.
Umuhimu wa utoaji elimu ya afya katika jamii ni kama ifuatavyo
1. Kupunguza gharama za matibabu , endapo kila mwananchi atafahamu na kuelewa jinsi ya kutunza mwili ataweza kuepukana magonjwa ambayo ingepelekea kutumia gharama kubwa katika matibabu.
2. Afya kuimarika , mwanajamii anaweza kuimarisha afya ambayo itamsaidia kufanya shughuli za kiuchumi au kijamii bila kusumbuliwa na magonjwa.
3. Kuongezeka /Kukua kwa maendeleo kupitia uwepo wa nguvu kazi- Magonjwa na afya duni hupelekea upotevu wa nguvu kazi jamii ikiweza kuimarisha afya itamudu kuzalisha na kuendesha shughuli za kiuchumi kwa kiwango kikubwa.
UMUHIMU WA UTOAJI ELIMU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA UMUHIMU WAKE KATIKA JAMII.
Elimu ya utunzaji wa mazingira inahusisha njia salama katika kuboresha vitu vinayvotuzunguka ikiwemo mimea,wanyama na visivyoviumbe hai.
NJIA ZA KUTUNZA MAZINGIRA.
1. Usafi wa maeneo yanayozunguka Majengo na maeneo ya wazi yasiyo na majengo. Mfano wa maeneo yanayozunguka shule,nyumba, hospitali na majengo mengine pia maeneo ya wazi ambayo hua na tabia ya kuota nyasi lazima yasafishwe kulinda uwepo mazalia ya wadudu .
2. Kuepuka utupaji wa taka ovyo au uchomaji wa plastiki , jamii inapaswa kupewa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa kujua namna ya kuhifadhi/kufukia taka ili kutunza mazingira.
3. Utunzaji wa maua na miti inayotoa kivuli au hata kupendeza ni moja ya elimu safi ya utunzaji wa mazingira
Utoaji wa elimu hizi husaidia kwa kiwango kikubwa jamii kujilinda dhidi ya magonjwa na maendeleo katika taifa.
Afya na mazingira ndio muhimili wa maendeleo mwanajamii hawezi kufanya shughuli za kiuchumi au kuzalisha bila ya uwepo wa afya bora na mazingira safi.
NJIA RAHISI ZA KUTOA ELIMU KWA JAMII.
1. Kuandaa matamasha ,mashindano michezo inayohamasisha jinsi ya utunzaji wa mazingira katika jamii zetu
2. Kuandaa machapisho,magazeti,majarida na makala zinazohamasisha utunzaji wa mazingira na afya.
3. Kuunda klabu,vikundi na vyama vinavyohamasisha na kutunza mazingira Katika taasisi na jamii.
4. Kuunda kampeni,sera zitakazohamasisha jamii kutunza mazingira na afya ya mwili.
Wito;Serikali, taasisi,mtu binafsi na jamii kwa ujumla kuzingatia usafi wa afya na utunzaji wa mazingira katika jamii kwa maendeleo ya taifa

Upvote
1