Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA VIJIJINI MWETU UNAENDELEA KUBORESHWA - WANAVIJIJI WAPEWA ZAWADI ZA KRISMASI
Utoaji wa Huduma za Afya ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini unaendelea kuboreshwa.
Ratiba za uzinduzi wa utoaji wa Huduma za Afya vijijini mwetu:
(i) Tarehe 6.12.2024
Zahanati ya Kijiji cha Nyabaengere ilianza kutoa Huduma za Afya
(ii) Tarehe 20.12.2024
Zahanati ya Kijiji cha Nyasaungu itaanza kutoa Huduma za Afya
(iii) Tarehe 23.12.2024
Kituo cha Afya Makojo kitaanza kutoa Huduma za Afya
Tunaishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kutupatia zawadi kubwa za Krismasi ya mwaka huu!
Uzinduzi mwingine uliofanyika mwaka huu:
(iv) Tarehe 10.10.2024
Kituo cha Afya cha Kisiwani Rukuba, Kata ya Etaro
(v) Tarehe 20.3.2024
Kituo cha Afya cha Kata ya Kiriba, kimejengwa Kijijini Bwai Kwitururu
Huduma za Afya Jimboni mwetu (Kata 21 zenye Vijiji 68) zinatolewa kwenye:
(i) Hospitali ya Halmashauri/Wilaya
(ii) Vituo vya Afya vitano (5)
(iii) Zahanati 24 za Serikali & 4 Binafsi
Ujenzi wa Zahanati mpya 17:
Wanavijiji wanaendelea na ujenzi wa zahanati za vijiji vyao. Baadhi ya hizo zahanati tayari zimeanza kupokea michango mikubwa ya fedha kutoka Serikali Kuu
Uzinduzi wa utoaji wa Huduma za Afya kwenye Zahanati mpya ya Kijiji cha Nyabaengere, Kata ya Musanja:
Tafadhali sikiliza VIDEO/CLIP kutoka Kijijini Nyabaengere
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Ijumaa, 13 Dec 2024