Wana ukumbi..matokeo ya Kidato cha nne kwa mwaka 2012 yamepokewa kwa hisia kubwa kwa Watanzania wote..Wazazi, Ndugu na Jamaa pamoja na watahiniwa wenyewe. Matokeo haya yameleta taswira mkanganyiko kwa watahiniwa wenyewe.
Taarifa za kushtua zilizopatikana ni kuwa vijana watatu (3) wamejiua kutokana na kufanya vibaya kwenye mitihani yao hii. Ombi langu ni kuwa tahadhari ya hali yajuu haina budi kuchukuliwa wakati wa kutoa taarifa za matokeo kwa wahusika. Hali ilivyo inabidi ifanyike Kanseling ya hali ya juu sana kabla hujatoa majibu. Kanselling sawa na ile anayofanyiwa mtu anayekwenda kupewa majibu ya UKIMWI...otherwise tutazidi kupoteza watu.
Huu ni msiba mkubwa. Vijana waelezwe kabisa kama majibu yanaweza yakawa mazuri au mabaya hivyo wayapokee tu..na hata yakiwa mabaya inawezekana ukajiendeleza na mambo yakawa mazuri. Au pia ule msemo maarufu wa kufeli masomo sio kufeli maisha waelezwe.