Hivyo vitu vinafanyika labda miaka hii vyuoni wameacha. Nakumbuka pale UDSM watu wa kozi mbalimbali utaona wako bize kwa ajili ya assignment mbalimbali walizopewa lengo ni kuwawezesha wasome references mbalimbali na kujiweka sawa. Pia kuna vipindi vya seminar mbalimbali ambazo wanafunzi wanachagua topics za presentation. Suala wengi wao kukopi kazi za wenzao hasa kwa zile kozi ambazo wanfunzi utakuta zaidi ya 100 ni vigumu lecturer kutoa assignment za kupresent au kuandika paper kwa mtu mmojammoja. Ila nakubaliana na wewe lectures pia wabadilike katika ufundishaji kwa mfano wawe wanatumia reserch papers mbalimbali kama mifano katika kufundisha na unaweza ukawapa wanafunzi hizo wazijadili hii itawajengea wanafunzi uwezo wa kujenga hoja hata ya kuwa karibu nauandishi wa research na hata kuvutiwa kutafuta research paper mbalimbali kwa mada husika na kusoma. Pia itawasaidia kujenga wazo na hisia na kufanyia kazi wazo hilo hata baada ya masomo