A
Anonymous
Guest
Nina kero yangu ya muda mrefu sana, mimi ni muajiriwa lakini pia ni mfanyabiashara ambaye nimefungua duka la vinywaji kwenye Soko la KIGILAGILA lililopo Kata ya Yombo Kiwalani Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Kero yangu kubwa na Wafanyabiashara wenzangu ambao tuna vizimba ni ujanja unaofanywa na wanaokusanya ushuru (kodi) ya vizimba hapa sokoni.
Mfanyabiashara wa fremu natakiwa kulipa Sh. 1500/= kwa siku lakini napewa risiti ya Sh. 1,000/= alafu napewa tena risiti ya Sh. 500/= hakuna risiti ya Sh. 1500/= moja kwa moja...
Juzi nimelipa kodi ya siku 15 kwa Sh 1,500/= ambapo nimetoa 22500/= lakini risiti niliyopewa imeandikwa siku 45 kiasi 500/= inamaana 500 × 45 days = 22500/= lakini ikifika siku 15 wanakuja tena kunidai wakati risiti wametoa imeandika siku 45.
Nimejaribu kufatilia kwa wenzangu nao nakuta wanapewa risiti sio kama mimi nimejaribu kuuliza kwa Mwenyekiti wa Soko hana majibu mwisho wa siku naambiwa nikijifanya mjuaji sana nitatolewa kwenye kizimba.
Naomba malalamiko haya yawafikie wahusika mana kuna soko la BOM BOM wao ni soko la manispaa kama sisi lakini wao tayar bei ya vizimba imeshashuka mpaka elfu moja kwa siku lakini soko letu bado.