Utofauti wa Clinical Officer na Medical Doctor.

Kulupango

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2020
Posts
288
Reaction score
535
Kuna tangazo radioni nilisikia chuo fulani wakitangaza kozi za clinical medicine kama Udaktari ngazi ya diploma. Baadhi ya watu wakaingia kwenye mabishano juu ya hilo.
Navyoelewa mimi Kozi yao inaitwa "Clinical medicine" yaani (Utabibu wa tiba ya kitaalam)
Ambapo anaesomea kozi hiyo kwa ngazi ya cheti huitwa Tabibu msaidizi (Clinical Assistant). Anaesomea kozi hiyo hiyo kwa ngazi ya Diploma huitwa "Afisa Tabibu" au Tabibu" yaani (Clinical Officer)

Hawa watu kwa jina moja hufahamika kama (Clinician) yaani Tabibu. Ambao kazi yao kubwa ni Kutibu mgonjwa ngazi ya kwanza (frontline health worker)

Sasa kielimu kuna utofauti kati ya Tabibu na Mganga.

Mganga ni yule aliesomea masomo hayo hayo ya clinician lakini ameyasoma kwa mapana zaidi na muda mrefu zaidi, huyu Mganga kitaalamu hufahamika kama "Physician" ambae kozi yake anayosemea hufahamika kama "Medical Doctor"
Akiwa mwaka wa kwanza huitwa MD1, MD2 MD3 MD4 MD5, akihitimu ndio huitwa "Physician" kitaalam. Au huitwa "Medical Doctor" yaani "mganga wa tiba ya kitaalam"

Sasa ni upi utofauti wa Clinician na Physician.
Ukigoogle utakuta wote wana kazi moja ambayo ni Kutibu, lakini physician kuna vitu vya ziadia kwake.

Lakini kwa uwelewa wangu
Mganga ni tofauti na Tabibu, Mganga anaweza kuwa tabibu lakini tabibu hawezi kuwa mganga.

Tabibu anahusika na magonjwa ya kawaida ambapo akikutana na magonjwa complex yakimshinda magonjwa hayo ndio huyaelekeza kwa mganga (refferal). Kwasababu mganga anavipimo vingi pia ana vifaa vingi kuliko Tabibu na anaelimu kubwa zaidi kuliko Tabibu.

Mwisho.
Kwangu mimi aliesomea kozi ya Clinical Medicine yaani Tabibu kujiita Daktari ni sawa kwasababu wote wanafanya kazi moja. Na kujiita kwake Daktari sio kujiita Medical Doctor bali atajiita Clinical Doctor ambayo hii ni kozi yao ya Degree kwa ngazi ya Clinical medicine inayoitwa (Bacheler of science in Clinical Medicine).

Screenshot_20200327-020512.png
Screenshot_20200327-020436.png
Screenshot_20200327-020703.png
 
Sekta ya afya nayo ina vikitu vingi sana... nadhani ndo sekta yenye mgawanyo wa vikolombwezo vingi kuliko sekta nyingine tulizozizoea mfano elimu ulinzi kilimo na mifugo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na usisahau kusema kuwa kozi za matabibu(clinical officer and assistant CO) zipo Tz tu

xi xhua tumzgunch
 
Kuna tangazo radioni nilisikia chuo fulani wakitangaza kozi za clinical medicine kama Udaktari ngazi ya diploma. Baadhi ya watu wakaingia kwenye mabishano juu ya hilo.
Navyoelewa mimi Kozi yao inaitwa "Clinical medicine" yaani (Utabibu wa tiba ya kitaalam)
Ambapo anaesomea kozi hiyo kwa ngazi ya cheti huitwa Tabibu msaidizi (Clinical Assistant). Anaesomea kozi hiyo hiyo kwa ngazi ya Diploma huitwa "Afisa Tabibu" au Tabibu" yaani (Clinical Officer)

Hawa watu kwa jina moja hufahamika kama (Clinician) yaani Tabibu. Ambao kazi yao kubwa ni Kutibu mgonjwa ngazi ya kwanza (frontline health worker)

Sasa kielimu kuna utofauti kati ya Tabibu na Mganga.

Mganga ni yule aliesomea masomo hayo hayo ya clinician lakini ameyasoma kwa mapana zaidi na muda mrefu zaidi, huyu Mganga kitaalamu hufahamika kama "Physician" ambae kozi yake anayosemea hufahamika kama "Medical Doctor"
Akiwa mwaka wa kwanza huitwa MD1, MD2 MD3 MD4 MD5, akihitimu ndio huitwa "Physician" kitaalam. Au huitwa "Medical Doctor" yaani "mganga wa tiba ya kitaalam"

Sasa ni upi utofauti wa Clinician na Physician.
Ukigoogle utakuta wote wana kazi moja ambayo ni Kutibu, lakini physician kuna vitu vya ziadia kwake.

Lakini kwa uwelewa wangu
Mganga ni tofauti na Tabibu, Mganga anaweza kuwa tabibu lakini tabibu hawezi kuwa mganga.

Tabibu anahusika na magonjwa ya kawaida ambapo akikutana na magonjwa complex yakimshinda magonjwa hayo ndio huyaelekeza kwa mganga (refferal). Kwasababu mganga anavipimo vingi pia ana vifaa vingi kuliko Tabibu na anaelimu kubwa zaidi kuliko Tabibu.

Mwisho.
Kwangu mimi aliesomea kozi ya Clinical Medicine yaani Tabibu kujiita Daktari ni sawa kwasababu wote wanafanya kazi moja. Na kujiita kwake Daktari sio kujiita Medical Doctor bali atajiita Clinical Doctor ambayo hii ni kozi yao ya Degree kwa ngazi ya Clinical medicine inayoitwa (Bacheler of science in Clinical Medicine).

View attachment 1400365View attachment 1400366View attachment 1400367
Kwa nionavyo mimi na uzoefu wa kwenda Hospitali, clinical ofisa ni mkubwa sana kuliko medical doctor, mara nyingi unakuta clinical oficer ni mtu mzima ana uzoefu na akikutibu unapona. wanajua sana. medical oficer ni watoto, hawana uzoefu na maara nyingi hata wakikutibu huponi lazima mwisho wa siku uende kwa clinical oficer
 
Ndugu yangu kutibu ni fani ya ubunifu, kutibu havihusiani na elimu ya mtu bali ni ubunifu na uzoefu wa mtaalam, hawa wanaosomea Clincal Medicine" mara nyingi ni wale waliofeli form six, na kutumia vyeti vya form 4 kuingia kwenye fani, wako vizuri wengi wao maana wao ni practical zaidi kuliko theory.
 
Mkuu hapa sisi wengine ni ngumu kuelewa ila nikimuona tu mtu kavaa overcoat jeupe tunajua ndiyo doctor mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Clinical Officer wengi utawakuta kwenye zahanati na vituo vya afya au hospitali za wilaya, au zile za mashirika binafsi wanawapenda sana, nafikiri kwasababu ni cheep kuliko MD.
 
Kama zilivyo taaluma nyingi zenye ngazi ya certificate hadi degree ndivyo ilivyo kwa taaluma ya Uganga hapa Tanzania; zingatia nitakavyofafanua

Mganga au tabibu mwenye Certificate huitwa Clinical Assistant na hawa mara nyingi level yao ya kutibu ni dispensary (Zahanati ) na Huishia Health centers (vituo vya afya ) hii kozi husomwa miaka 2 na sifa za kujiunga ni form four mwenye angalau alama D kwa masomo ya physics, chemistry na biology.

Mganga au tabibu mwenye Diploma huitwa Clinical officer na hawa mara nyingi level yao ya kutibu ni dispensary (Zahanati), Health Center (Vituo vya Afya ) na Huishia hospitali za wilaya. Kozi hii husomwa miaka 3 na sifa za kujiunga ni form 4 mwenye alama D katika masomo miwili kati ya yale 3 ya Sayansi na C kwa somo moja wapo.

Mganga au tabibu mwenye degree huitwa Medical doctor au MD hawa mara nyingi level yao ya kutibu ni hospital za wilaya,hospital za mkoa na zile za rufaa, sifa za kujiunga ni form six aliyefaulu masomo ya mchepuo wa PCB angalau DIV ONE, I Mean CCC. DV 2 Ni mara chache kuchaguliwa. Hawa huchukua miaka 6 kumaliza mafunzo yao. Na kuanzia level hii wengine huenda kusoma miaka mitatu au zaidi ili kuwa Physician (sijui kiswahili yake),Surgeon( Bingwa upasuaji), Paediatric (Bingwa watoto), Gynaecologist (Bingwa wanawake) n.k

NB: Clinical Officer anaweza kujiendeleza hadi kuwa Medical Doctor pia kati ya CO na MD kuna kozi ya miaka 2 inayoitwa AMO yaani Assistant Medical Doctor, mwaka jana 2019 ilifutwa rasmi.
 
Kwa hiyo kwa mtazamo wako CA na CO kujiita Madokta ni sawa!?
 
Hawa jioni Madaktari ila wagonjwa ndio huwaita hivyo, mfano kwa akili zako nyingi ikitokea unamkuta CA katika katika kituo cha huduma akijitambulisha kwa mgonjwa kuwa yeye ni daktari mahali pale ikiwa ni katika mazungumzo na mteja wake, unafikiri atakuwa akakosea?
 
Ndugu yangu kutibu ni fani ya ubunifu, kutibu havihusiani na elimu ya mtu bali ni ubunifu na uzoefu wa mtaalam, hawa wanaosomea Clincal Medicine" mara nyingi ni wale waliofeli form six, na kutumia vyeti vya form 4 kuingia kwenye fani, wako vizuri wengi wao maana wao ni practical zaidi kuliko theory.
Practical kuliko theory aisee!! Hivi utakuaje vizuri kama umeshidwa kufaulu biology ya fom 6? Wabongo tuache uvivu, rudi darasan kasome uwe MD na sio ukae hapo ujifariji na kujificha kwenye kichaka cha "practical zaidi kuliko theory" huo ni ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama zilivyo taaluma nyingi zenye ngazi ya certificate hadi degree ndivyo ilivyo kwa taaluma ya Uganga hapa Tanzania; zingatia nitakavyofafanua

Mganga au tabibu mwenye Certificate huitwa Clinical Assistant na hawa mara nyingi level yao ya kutibu ni dispensary (Zahanati ) na Huishia Health centers (vituo vya afya ) hii kozi husomwa miaka 2 na sifa za kujiunga ni form four mwenye angalau alama D kwa masomo ya physics, chemistry na biology.

Mganga au tabibu mwenye Diploma huitwa Clinical officer na hawa mara nyingi level yao ya kutibu ni dispensary (Zahanati), Health Center (Vituo vya Afya ) na Huishia hospitali za wilaya. Kozi hii husomwa miaka 3 na sifa za kujiunga ni form 4 mwenye alama D katika masomo miwili kati ya yale 3 ya Sayansi na C kwa somo moja wapo.

Mganga au tabibu mwenye degree huitwa Medical doctor au MD hawa mara nyingi level yao ya kutibu ni hospital za wilaya,hospital za mkoa na zile za rufaa, sifa za kujiunga ni form six aliyefaulu masomo ya mchepuo wa PCB angalau DIV ONE, I Mean CCC. DV 2 Ni mara chache kuchaguliwa. Hawa huchukua miaka 6 kumaliza mafunzo yao. Na kuanzia level hii wengine huenda kusoma miaka mitatu au zaidi ili kuwa Physician (sijui kiswahili yake),Surgeon( Bingwa upasuaji), Paediatric (Bingwa watoto), Gynaecologist (Bingwa wanawake) n.k

NB: Clinical Officer anaweza kujiendeleza hadi kuwa Medical Doctor pia kati ya CO na MD kuna kozi ya miaka 2 inayoitwa AMO yaani Assistant Medical Doctor, mwaka jana 2019 ilifutwa rasmi.
Umemalizia uzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom