Utofauti wa mgeni kutoka mjini kwenda vijijini na mgeni kutoka kijijini kwenda mjini

Utofauti wa mgeni kutoka mjini kwenda vijijini na mgeni kutoka kijijini kwenda mjini

madeinmusoma

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
324
Reaction score
387
MGENI KUTOKA MJINI

Upo mjini mfano tuseme Dar es Salaam unapiga simu kijijini kuwa unaenda kuwasalimia wanafurahi sanaa. Inafika siku ya safari haukauki midomoni mwao wakizungumzia ujio wako.

Unafika stendi unakuta familia nzima inakusubiri kwa bashasha kila mmoja anataka apige stori na wewe mnafika nyumbani unakuta umechinjiwa kuku chakula cha kutosha. Hapo wanatamani wasilale kila mmoja akikuuliza swali hili na lile lakini wakiwa na furaha kukuona. Inafika asubuhi kama kuna wanao soma wanatamani wasiende shule ili wabaki na wewe.

Ikifika siku ya kuondoka sasa usiombe iwe Mbeya utafungiwa mpunga wa kutosha kuku kama wote na mazaga kibao kama vile wewe ndie mfalme wa ukoo, watakusindikiza ukoo mzima hadi stendi kwa furaha kubwa hadi unaondoka.
Mwenyezi Mungu awabariki muishio kijijini.


MGENI KUTOKA KIJIJINI KUJA DAR.
Upo kijijini unapiga simu ya kwenda kusalimia Dar utajibiwa karibu sana. Unapanda gari unafika stendi hukuti mtu unapiga simu utaambiwa angalia hapo kushoto kuna bajaji chukua tutalipa.

Unapanda bajaji hadi nyumbani piga hodi anatumwa mfanya kazi kukupokea unapoingia ndani utaambiwa na mama mwenye nyumba kariiibu huku akiwa anachati, unajibu kwa furaha asante. Mara unaona vitoto vipo bize na kucheza gemu vitaambiwa mbona hamsalimii ndipo utasikia shikamooo huku viko bize na game. Mara utasikia anaitwa mfanyakazi akupe chakula ukiwa unaendelea kula unakuta kila mmoja yupo bize vitoto vinacheza game, mama yupo Facebook,Twitter na WhatsApp anachati halafu kumbuka siku hizi kuna TikTok. Unakula ukipumzika kidogo anaitwa mfanya kazi akuoneshe chumba cha kulala.

Ikifika siku ya kuondoka zitachambuliwa nguo wasizovaa, zimechakaa kidogo au zinawabana wanakujazia wewe. Inafika asubuhi anaitwa bodaboda kukuchukua na kukupeleka stendi kisha unarudi kijijini kwenu.

Huo ndio utofauti wa MGENI KUTOKA mjini kwenda vijijini na MGENI kutoka kijijini kwenda mjini [emoji2772][emoji1732]
 
Back
Top Bottom