UTONGOZAJI WA WATUMISHI WA BWANA

Snipperkilungu

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
253
Reaction score
424
Mtumishi :
Hello Binti Bwana asifiwe

Binti:
Amen mtumishi

Mtumishi :
mrembo, samahani, una mpenzi?

Binti:
Hapana. Sina mpenzi.

Mtumishi:
nakupenda Binti tuishe wote Kama mke na mume , Kitabu cha Mwanzo 2: 18 "Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye."

Binti:
Lakini mimi sikupendi jamani!!!

Mtumishi:
Waraka wa kwanza wa Yohana 4:8 "Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo."

Binti:
Mh!! Mi ntajuaje kwamba na wewe unamaanisha hayo maneno?

Mtumishi:
Injili ya Mathayo 12:34b "Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake."

Binti:
Jamani leo kazi ninayoi!!. Mi ntajuaje kwamba we ni mkweli na mwaminifu?

Mtumishi:
Injili ya Marko 13:31 "Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe."

Binti:
Wewe! Na kwanini umekuja kwangu? Wasichana mbona wako wengi tu!

Mtumishi:
Mithali 31:29 "Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote."

Binti:
We una mambo wewe!! Sasa mimi kwangu umependa kitu gani?

Mtumishi:
Wimbo Ulio Bora 4:7 "Mpenzi wangu, u mzuri pia, Wala ndani yako hamna ila."

Binti:
Mh! Huo uongo, mbona mimi hata sio mzuri kihivyo. Unaongeza chumvi tu!

Mtumishi:
Mithali 31:30 "Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa."

Binti:
Nikisema nimekukubalia itakuaje!?

Mtumishi:
Mwanzo 2:24 " Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja."

Binti:
Jamani we mkaka., Inakuaje unajua maandiko kiasi hicho?

Mtumishi:
Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana."

Binti:
Wowwww! Naona unampenda sana Mungu.

Mtumishi:
Zaburi 34:8 "Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini."

Binti:
Mh! Haya bwana. Basi nipe muda nifikirie ombi lako.

Mtumishi:
Wafilipi 4:8 "Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo."

Binti:
Mh! Jamani wewe, haya, nimekubali. Mpaka hapo nimekupenda na nipo tayari kuolewa na wewe !!

Mtumishi:
Ufunuo wa Yohana 22:21 "Amina"
 
AZINIYE NA MWANAMKE HANA AKILI KABISA...
 
Haya ubarikiwe saana kwa kuwafundisha hao madomo zege wasiokuwa na uwezo wa kumsomesha mwanamke hadi alitumie vibaya neno la uzima. Uliona shida gani kusema walokole ukaona uwaseme watumishi wa bwana?
 
Mpendwa katika ubora wake
 
Daaaaaa umenikumbusha nikiwa mwenyekiti wa tycs nilivyo tumia njia hiyo kupiga papuchi
 
Basi ngoja nichukue hizi verse nikamtokee yule binti mlokole maana nilikua sina swagger
 
Haya ubarikiwe saana kwa kuwafundisha hao madomo zege wasiokuwa na uwezo wa kumsomesha mwanamke hadi alitumie vibaya neno la uzima. Uliona shida gani kusema walokole ukaona uwaseme watumishi wa bwana?
Hajalitumia vibaya Neno. kama nia yake ni kupata Mke, basi njia hiyo ni sahihi ya kunukuu maandiko matakatifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…