Utopolo mbona mnayakana maneno yenu?

ITR

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
6,096
Reaction score
16,390
Shujaa muongoza njia alishatahadharisha kuwa tuogope sana Mungu na teknolojia.

Kauli ya kombe la shirikisho ni kombe la walioshindwa na vilaza ni kauli iliyo tolewa na msemaji wa utopolo na mashabiki wakaushikia bango msemo huo , na ndo ulikuwa wimbo wao mwaka jana kipindi simba inacheza michuano hiyo.

Lakini sasa hivi ukisema utopolo anashiriki kombe la walioshindwa na vilaza mashabiki wa utopolo wanatamani wakurukie na kukumeza.

Sasa mnacho kataa ni kipi na mnacho kubali ni kipi? Ya kwamba muliliita kombe la vilaza kwa sababu simba ndo alikuwa mshiriki ila baada ya nyinyi kushiriki ndo limekuwa kombe la maana?
Au kombe alilo shiriki simba mwaka jana lina tofauti na la mwaka huu ambalo mnashiriki nyinyi?

Kwakweli kocha wenu alikuwa sahihi kwa kuwaita manyani maana akili zenu ni zakinyani kweli.

Aisee tekinolojia ni kitu cha kuogopa sana ona sasa hivi inavyo wahukumu na kuwaumbua utopolo yapo yana tapatapa haya jui yashike wapi, na hayo maneno yenu yatawahukumu mpaka mwisho wa dunia hii.

Utopolo na unafiki ni sawa na maji na samaki huwezi kuwatenganisha.
 
Aliyewaita mbumbumbu kweli alikuwa sahihi kwa 100%. Na kama kuna uwezekano wa kujengewa sanamu ya kumbukumbu, ingependeza zaidi. Na binafsi nipo tayari kuchangia chochote kitu kwenye huo ujenzi.

Kwa hiyo kila kitu anacho/alichowahi kusema huyo mropokaji, na mwanachama wenu aliyewahi kuajiriwa na GSM baada ya kukimbia mshahara kiduchu wa laki 7 kwa mwezi, ndiyo msimamo wa klabu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…