Tarehe 15/10/2013 idadi kubwa ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Dunda waamua kutohudhuria shule baada ya kujiamulia kukaa nyumbani.Shule hii ipo mkoa wa Pwani wilaya ya Bagamoyo. Wanafunzi waliohudhuria walikuwa 25 katika ya wanafunzi 500 na ushee.Mgawanyiko wa mahudhurio ya wanafunzi hao ni kama ifuatayo: form one 10, form two 5,form three 3 na form four wawili.Hata hao waliobaki waliamua kutoroka wote baada ya mapumziko.Hali hii ilipelekea shuleni kubaki walimu tu waliokuwa tayari kuwafundisha wanafunzi hao. Kwa muda mrefu shule hii imekuwa inakabiliwa na utovu wa nidhamu wa hali ya juu ikiwemo utoro,wanafunzi kuwapiga na kuwatukana walimu,vitendo vya uesharati vya wanafunzi pamoja na kukesha katika kumbi za starehe kama Rusona ya Bagamoyo. Vitendo hivi viovu vya wanafunzi vinapelekea kushuka kwa taaluma ya shule hiyo,kwani matokeo ya kidato cha nne ya shule hiyo ni mabaya mno miaka yote. Malengo ya Big Results Now kwa shule hiyo yanaweza kuwa Big Results No.Mh.Waziri Sh ukuru Kawambwa okoa shule ya jimbo lako na kata yako.