Utoro uliokithiri : Shule yabaki na walimu tupu.

mbeyaman

Member
Joined
Sep 28, 2013
Posts
97
Reaction score
28
Tarehe 15/10/2013 idadi kubwa ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Dunda waamua kutohudhuria shule baada ya kujiamulia kukaa nyumbani.Shule hii ipo mkoa wa Pwani wilaya ya Bagamoyo. Wanafunzi waliohudhuria walikuwa 25 katika ya wanafunzi 500 na ushee.Mgawanyiko wa mahudhurio ya wanafunzi hao ni kama ifuatayo: form one 10, form two 5,form three 3 na form four wawili.Hata hao waliobaki waliamua kutoroka wote baada ya mapumziko.Hali hii ilipelekea shuleni kubaki walimu tu waliokuwa tayari kuwafundisha wanafunzi hao. Kwa muda mrefu shule hii imekuwa inakabiliwa na utovu wa nidhamu wa hali ya juu ikiwemo utoro,wanafunzi kuwapiga na kuwatukana walimu,vitendo vya uesharati vya wanafunzi pamoja na kukesha katika kumbi za starehe kama Rusona ya Bagamoyo. Vitendo hivi viovu vya wanafunzi vinapelekea kushuka kwa taaluma ya shule hiyo,kwani matokeo ya kidato cha nne ya shule hiyo ni mabaya mno miaka yote. Malengo ya Big Results Now kwa shule hiyo yanaweza kuwa Big Results No.Mh.Waziri Sh ukuru Kawambwa okoa shule ya jimbo lako na kata yako.
 
tarehe 15 ilikuwa sikukuu, hata makazini nilikuwa na utoro...
 
Kupumzika nayo imo bhana...
Saa zingine shule inachosha sana, acha vijana wajipe kamid-term (friday-thursday)
 
Tulikua kwenye idd,wala si utoro.,leo tumefika shule ila waalimu hawapo na tupo 475 muda huu
 
Utovu wa nidhamu hilo ni jambo tofauti na mahudhurio kwa siku husika
Dunia yote wamesherehekea sikukuu siku hiyo, Siasa za Tanzania zimefanya sikukuu kuwa tarehe 16,

Tuwasaidie hao watoto kwa hilo la utovu wa nidhamu ili wapate ELIMU BORA
 
Utoro umesababishwa na mfumo kristo ha aha ha ha ha.
 

Kwani wewe hupendi mapumziko ya hiari? Kama hayahudhurii achana nayo as long as unapata salary sidhani kama hilo linakuhusu. ELIMU NI HAKI NA URITHI WA MTOTO, wao wameamua kurithi uvivu, ngoma na upuuzi mwingine ambao ni zao la jamii yao. Lawama kama hizi ipeni jamii kwa malezi ya hovyo isiyoona umuhimu kuwekeza ktk elimu kwa maendeleo ya Taifa na jamii yao kwa ujumla.
 

"Hekima" zako zimesomeka. Zitafanyiwa kazi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…