Utosi wa mwanangu haujakaza mpaka sasa

Utosi wa mwanangu haujakaza mpaka sasa

Mrs. Rama

Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
7
Reaction score
0
Habari za kazi wadau.

Naomba mnisaidie, mwanangu ana miezi kumi now lakini bado utosi wake unapiga.

Hili ni tatizo ama? na je nifanyeje ili utosi wake uache kupiga (ukaze)?
 
Tafuta wamasai wanaouza dawa za kienyeji kuna dawa ya kumpaka kichwani na nyingine anakunywa .ukiwaona hao au mabibi watamaliza tatizo hilo
 
Tafuta wamasai wanaouza dawa za kienyeji kuna dawa ya kumpaka kichwani na nyingine anakunywa .ukiwaona hao au mabibi watamaliza tatizo hilo

Mleta Mada Fuata Ushauri Wa Huyu Member
Kumbuka Kizazi Chetu Tumeweka Mbele Uzungu Na Kudharau Watu Kama Mabibi Wanajua Mengi Sana
 
Tafuta wamasai wanaouza dawa za kienyeji kuna dawa ya kumpaka kichwani na nyingine anakunywa .ukiwaona hao au mabibi watamaliza tatizo hilo
ntafanya hivyo mdau.., mana usijekuta badae ikaleta matatizo mengine bure...
 
Tafuta wamasai wanaouza dawa za kienyeji kuna dawa ya kumpaka kichwani na nyingine anakunywa .ukiwaona hao au mabibi watamaliza tatizo hilo

Acha upuuzi ndugu, nani kakwambia huyo mtoto ana tatizo? Kitaalamu utosi wa mtoto hufunga kabisa anapokuwa na miezi 18. Kwa hiyo hapo hamna tatizo lolote kwenye utosi.
Mtoa mada usifuate ushauri mbuzi kama huu, kama umeweza kuingia ktk mtandao na kupost mada hii basi naamini unaweza kutafuta uelewa zaidi kutoka mtandaoni kupitia source zinazoaminika. Pia kutembelea daktari wa watoto kama unahisi hujanielewa. Shukran
 
Back
Top Bottom