Utpeli wa kazi kupitia simu za mkononi sms

maju

Senior Member
Joined
Oct 20, 2011
Posts
118
Reaction score
28
Watanzania wenzangu kuna wizi mpya unaotumiwa na kampuni inayotoa huduma kushirikiana na makampuni yetu ya simu za mnkononi inayojitangaza kupitia radio ya clouds FM, kwamba wanauza magari, viwanja , kupangisha nyumba na kutafutia watu kazi.Utafiti uliofanyika umeonesha dhairi hii kampuni ni ya kitapeli na haina uwezo huo technically.

Hawa wahuni wanachofanya ni kumiliki namba ya SHORT CODE mfano; 155xx ect, ambayo hutolewa ana TCRA kisha kuisajili kwenye makampuni ya simu ili wagawane mapato kwa kila sms zipitiazo kwenye SHORT CODE hiyo (kila sms Tshs. 500). Kisha huitangaza kwa nguvu zote kwenye Radio station husika.

Mtanzania anayetuma sms huliwa pesa zake wakati hawa jamaa hawana hata database ya huduma husika, hata ofisi zao hawana hata miundombinu zaidi ya komputa ya muhudumu wa ofisi. Mwisho wa siku hawa jamaa hupitia kwenye makampuni ya simu kufuatilia sms zilizoingia ili wapate mgawo wao.

Nawasihi watanzania tuwe makini na hizi promosheni za wizi zinazopitia short code zitolewazo na tcra kwenye simu za mkononi. Na TCRA wawe makini na watu wanaowapatia hizi short code kwani watanzania wanazidi kuibiwa na hawa matapeli.
 
Thanks mkuu kweli inatangazwa kweli na ile inayo jiita radio ya watu.
 
Kwani katika ulimwengu huu wa teknolojia ya mawasiliano ofisi si inawezakuwa lap top yako tu?

Ukituma hizo sms hupati huduma yeyote? au inakuwaje?
 
sindio ile inajiita BR SOLUTION...... kweli ni matapeli sababu walishawai kunitapeli,nikafuatilia nikagundua hawana lolote.....
 
yani na akili zenu mnakaa kutuma msg kwa hao watu, uo utakua upungufu wa akili mwilini
Yaani io 500 yako ni bora ukanunue daily news utapata nafasi nyingi tu za kazi
kweli wajinga ndo waliwao
 
yani na akili zenu mnakaa kutuma msg kwa hao watu, uo utakua upungufu wa akili mwilini
Yaani io 500 yako ni bora ukanunue daily news utapata nafasi nyingi tu za kazi
kweli wajinga ndo waliwao

nAUNGA MKONO HOJA.
 
Yaan mi huduma yoyote inayotolewa na namba 15xxx situmii wana mambo ya ajabu sana yaan kuna huduma moja nilijiunga mwaka jana kila nikiacha hela kwenye simu wananitumia sms za ajabu wanakata hela yote nimejaribu kujitoa wananiambia watanitoa baada ya masaa 24 lakini hawanitoi wananikera balaa!
 
yani na akili zenu mnakaa kutuma msg kwa hao watu, uo utakua upungufu wa akili mwilini
Yaani io 500 yako ni bora ukanunue daily news utapata nafasi nyingi tu za kazi
kweli wajinga ndo waliwao

Naunga mwili mzima hoja 100%
 
Bora sisikilizi hiyo radio.

Thanx kwa taarifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…