Utu na utoaji!



Nakubaliana na wewe.
 
Watu wanaogopa hata kutoa damu nini figo. Hasa mtu akijua hajatulia anaogopa asijeambiwa afya haijatulia.
Kutoa figo sawa ila damu kwani mtu atapungukiwa nini??Labda hao unaosema wanaogopa wasijekutwa/julika wana ngoma ndo naweza kuelewa wanachokwepa ni nini!
 
Itategemea aisee hii ni ngumu sana inataka ujasiri
 
Kwaroho zetu binadamu najua jambo lakujitolea ni gumu sana kuingia akilini linashindikana la vitu kama pesa na chakula. Hadi mtu aone atanufaikaje kwa msaada anaoutoa.
Lizz, michelle mnadhani la viungo vya mwili litakuwa rahisi? Hiyo haipo unless further notes.
 

Lizzy! swalilako gumu sana, kirahisi naweza sema nitajitolea, lakini kiukweli itategemea litapotokea.. Watu tunakimbia hata kujitolea damu! kwa figo mmh, tuombe Mungu yasitukute kwani hapo tutatofautisha rangi saba bila mikwaruzo! Mungu epushia mbali.
 

nini figo lizzy, watu kujitolea damu tu huwa ni mtihani mkubwa.
 

Hivi utajisikiaje kusimama kaburini ukilia huku ukijua fika ungeweza kuisogeza siku hiyo mbele ila hukufanya hivyo??
 

Hao wanaokimbia hata kutoa damu wananichekesha kweli.Hua wanadhani itaishaa ama?
 

...huenda tukawalaumu ndugu wa huyo mheshimiwa, lakini hatujui kimewasibu nini mpaka wamesitisha kutoa huo ushirikiano. Huenda hawajapewa ushauri nasaha unaohitajika kwenye case kama hii. Tunadanganyana na kutishana as if ukijitolea figo yako, siku ukipata mushkeli basi ndio RIP hiyo...

Vile vile, lifestyle zinaweza kuwa zinachangia maamuzi ya hawa wanandugu. Who am I to judge them? ni wao na mwenyezi Mungu wao. Kuna msemo, what goes around comes around. Wenzetu kule India, biashara ya kuuza kidneys imeshamiri sana kiasi cha kupelekea black market ya viungo vya binadamu.

Binafsi na bad experience kipindi mzee wangu anaumwa (Cancer,) alikuwa anahitajika kuongezewa damu mara kwa mara. Kilikuwa ni kipimo tosha kwa wanandugu, jamaa na marafiki tutasaidianaje. Wengi walikuwa wanakimbia hata kutest kama Blood Groups zina match. Wengine siku ya kutoa damu waliingia mitini, na wengine kushawishiwa kwa 'mshiko!' ...Ilibidi baadhi warudie kuchangia damu kukidhi mahitaji ya mgonjwa.

Siku nikikumbwa na mtihani kama huu, Mw'Mungu ataniwezesha nguvu na imani nijitolee figo kuliko kumuona ndugu yangu akiteseka.
 
lIZZY, KUTOA FIGO NI RAHISI KAMA UKO NCHI ILIYOENDELEA, LAKINI KUTOA FIGO TANZANIA YAWEZA IKAWA NDIO MWISHO WA MAISHA YAKO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…