figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
1.Alitozwa Dola 400,000 (zaidi ya shilingi 700,000,000 ta kitanzania) kwa kwenda kwenye klabu ya uchi siku moja kabla ya mechi
2. Akiwa kwenye gari aina ya Bently, Januari mwaka 2012, Baloteli alisimama kwenye shule moja akiwa na marafiki zake, akatumia choo cha shule hiyo, kisha wakazunguka maeneo ya shule hiyo kwa dakika 20 na kuondoka.
3.akiwa na marafiki zake nyummbani wakirusha fataki za moto, Balotelli alitupa fataki moja bafuni na kuchoma bafu lake, askari wa zimamoto walikuja baadae na kuzima moto huo.
4. Akiwa Machester city, Kocha aliwahi kumtoa nje baada ya kukosa bao la wazi! Katika tukio hilo, Baloteli alibaki yeye na golikipa, na badala ya kufunga aligeuka na kuupiga kwa kisigino na kuutoa mpira huo. Kocha alimtoa nje dakika hiyohiyo.
5.Mtoto mdogo wa shule ya msingi alimwambia balotelli kuwa anaonewa sana shuleni, Balotelli alifunga safari na kwenda shuleni hapo ili kumpa moyo.
6.Alishawahi kumpa dola 1,000 ombaomba barabarani baada ya kushinda dola 25,000 kwenye kamali kwenye kasino moja mwaka 2011. Baada ya Kushinda fedha hizo, aliziweka kwenye kiti cha mbele cha gari yake huku akizunguka Mjini, askari walipomuuliza kwanini anaweka kiasi kikubwa cha pesa hadharani aliwajibu "Ni kwa kuwa naweza kufanya hivyo, hicho ndicho mnachotakiwa kujua"
7. Alikamatwa akiwa na ndugu yake, wakipita kwenye Gereza la wanawake nchini Italia mwaka 2010.
8.Alishawahi Kuiba Lenzi ya kamera ya Mwandishi wa Habari nchini Italia
9. Alipigwa Faini ya dola 100,0000 kwa kuwarushia wachezaji wenzake mishale ya Darts wakiwa mazoezini. alipouliza alijibu kuwa alikuwa na alikosa cha kufanya.
10. Alishawahi kushindwa kuvaa nguo ya mazoezi mpaka aliposaidiwa na Msaidizi wa klabu.
Chanzo: Blogs