SoC01 Utulivu huleta maamuzi sahihi kwenye kila jambo

SoC01 Utulivu huleta maamuzi sahihi kwenye kila jambo

Stories of Change - 2021 Competition

PJM87

Member
Joined
Aug 20, 2021
Posts
43
Reaction score
50
Habari zenu wadau .?

Mimi nitaandika kidogo kuhusu utulivu wa mtu na jinsi unavyoweza kumsaidia myu katika kuaminiwa, au kufanya jambo lolote lile katika maisha ya kila siku.

Ni maanaya utulivu.??
Utulivu kwangu mimi nasema ni ile hali ya mtu kujipa tafakari la muda kiasi utakao msaidia kufanya maamuzi anayoona kuwa nisahihi na kajiridhisha.


Umuhikmu wa utulivu katika maisha ya kila siku.

1. Utulivu huleta kuyafikia maamuzi sahihi.

Mtu unapokuwa na utulivu katika jambo lolote unalowaza au unalolifanya ni lazima utafikia maamuzi yaliyo sahihi na yatakayo kusaidia.

2. Utulivu huleta ubunifu.

Katika jambo ulitendalo utulivu ukiwelo lazima uweze kufanya ubunifu ndani yake.

3. Utulivu huleta kuaminiwa na kuaminika kwa watu na jamii yote ikuzungukayo.

Ni wazi ili watu wa jamii yako au popote ili uheshimike lazima uwe na utulivu kiasi cha kuonyesha jinsi unavyoweza kukabiliana na changamoto.

4. Utulivu huleta maelewano katika jamii.

Watu wa jamii moja wanapokuwa na utilivu katika shughuli yoyote waifanyayo lazima waelewane vizuri.

5. Utilivu ni subira yenye faida.

Mtu anapokuwa mtulivu anajijengea subira itakayo mpa faida katika maisha yake.

6. Utulivi pia ni tabia njema.

Utulivu pia ni tabia njema mbele za watu. Hususani unapokua katika shughuli mbalimbali za kijamii

7. Utulivu huleta mafanikio.

Utulivu unaleta mafanikio kote iwe kibiashara kimaamuzi, kiutafiti, kimichezo, kimalengo, nk

8. Utulivu hutusaidia kuyafikia malengo yetu.

Utulivu pia hutusaidia kuyafikia malengo tuyapangayo na kuyafanikisha maana utulivu hutuondolea panic nk


Hitimisho tuwe watulivu tutafanikiwa mengi

Msisahau kupigia kura pia andiko hili
 
Upvote 2
Back
Top Bottom