SoC04 Utumishi kwenye Kata na Tanzania tuitakayo

SoC04 Utumishi kwenye Kata na Tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
May 7, 2024
Posts
6
Reaction score
2
Screenshot_20240515-231328_1.jpg

Imekua ni dhana iliyoko kwenye vichwa vya watu wengi hasa watumishi, wapya na wengine wazoefu kuwa kufanya kazi kwenye kata ni jambo gumu sana kuweza kulitekeleza, na hiyo inathibitika kutokana na hali ilivyo katika kata nyingi nchini Tanzania. Watumishi wengi wanaofanya shughuli zao kwenye kata wamekua wakitoa malalamiko mengi sana kiasi cha kuwaogopesha watu wengine wanaotegemea kupata ajira, na kuwatengenezea picha mbaya ya mazingira watakayo kutana nayo kwenye kata pindi watakapo pata ajira. Vile vile suala hili si nadharia linathibitika kuwa mazingira ya baadhi ya kata kiutumishi ni magumu sana hali inayopelekea watumishi wengi wanaofanya kazi katika kata kuonekana kutokubaliana na maeneo hayo ya kazi.

Ni ukweli usiopingika utumishi katani ni mgumu. Hawa ni baadhi ya watumishi wanaofanya kazi kwenye kata.

•Afisa mtendaji wa kata/ kijiji
•Walimu wa sekondari na shule za msingi / Afisa elimu kata
•Watumishi wote wa idara ya afya wa vituo vya afya vya kata
•Maafisa kilimo, mifugo na uvuvi
•Afisa maendeleo ya jamii
•Polisi kata nk

Watumishi hawa wamekua wakikumbana na changamoto kadha wa kadha katika utumishi wao katani, ikiwa yafuatayo ni baadhi tu,

•Kukosekana kwa makazi,(nyumba) kwa baadhi ya watumishi. Idara ya afya,polisi na elimu imejipambanua kwa asilimia chache mno kujenga nyumba za watumishi, na hata nyumba chache zilizopo hazina ubora na hazikidhi vigezo na viwango vya watumishi hawa.

•Kukosekana kwa nyenzo za usafiri kama vile (pikipiki, gari nk) kwa lengo la kutekeleza majukumu ya kata. Katika kata zingine itamgharimu mtumishi kusafiri zaidi ya kilomita 70 Kwa garama zake Ili kufanya kazi ya kata, ni ama amewasilisha taarifa halmashauri au kwenda kwenye maeneo mengine ndani ya kata, jambo hili linapelekea umaskini na madeni (kausha damu) kutajwa sana Kwa watumishi wengi wanaotumika katika kata.

•Kutofidiwa muda wa ziada wa kazi(overtime). Watumishi wengi wa kata wanatumia msemo unaosema "serikali imefumba macho yao kwao" hii inatokana na juhudi wanazozifanya hata nje ya muda kutochukuliwa ukubwa na kukosa haki zao za malipo maarufu kama "overtime"

•Posho. Hili neno limebeba maana kubwa sana kwenye utumishi, na wanaonufaika ngazi ya kata ni asilimia ndogo mno, watumishi wengine hupita mwaka bila kupata posho yoyote au kupata kazi itakayompatia posho. Na kama tunavyofahamu mishahara haiwezi kukidhi haja zote za watumishi.

•Uchakavu wa Ofisi. Asilimia kubwa ya Ofisi za kata ni CHAKAVU na serikali hainyeshi jitihada za karibu za kutaka kuboresha mazingira ya Ofisi za watumishi katani,"ikimbukwe ubora wa Ofisi ni Moja ya motisha kazini" Ofisi hizi ni hatarishi Kwa watumishi, ziko Ofisi zinazofuga wadudu kama vile buibui, popo, panya,hata mara pengine nyoka kutokana na uchakavu wa Ofisi za kata. Vile vile miundombinu mibovu hutajwa kwenye kata, takwimu zisizo rasmi Ofisi nyingi za kata hazina umeme hivyo haziwezi kutumia vifaa janja kama kompyuta nk.

•Dhihaka. Watumishi wengi wa kata wamekua wakidhihakiwa, ikiwa ni ukatili wa kisaikilojia kutoka kwa baadhi ya watu(watumishi na wasio watumishi). Maneno hayo ya maudhi wameshusha motisha ya watumishi wengi hasa waalimu na watendaji," ikimbukwe mtendaji wa kata akidhihakiwa mapato yatashuka ".

MAWAZO YANGU.
•Serikali kupitia Wizara zinazoajiri zipange bajeti ya kununua vifaa, kama vile simu, pikipiki na kompyuta mpakato, kwajili ya watumishi wa kata, ambavyo ikiwa mtumishi atapangiwa kwenye kata lazima akabidhiwe hivyo. Namba ya watu watakao ajiriwa itokane na vifaa vilivyotengwa kwa kipindi husika.

•Serikali itoe gari moja kwenye kila kata, litakalosimamiwa na mtendaji wa kata, huku likifanya shughuli za maendeleo ya kata bila kubagua.

•Serikali iongeze mishahara kwa watumishi wa kata kama moja ya utumishi wao, Ili kuongeza ufanisi kwa watumishi wa kata.

•Nyumba za watumishi zijengwe zenye hadhi ya watumishi mahali popote. Hii itasaidia si tu kuongeza ufanisi kwa watumishi bali hata kukuza kata.

•Vifaa vya kielekroniki viwepo kwenye Ofisi za kata Ili kusaidia kutunza kumbukumbu na kutuma taarifa kwa haraka na kwa ufanisi.

•Wataalamu wa Sheria walatwe kwenye kata, maana uvunjifu wa haki huanzia kwenye kata, na watendaji kata wengi hawana elimu ya sheria. Vifo na chuki huanzia huko maana mashamba yako huko na ndipo wanapodhulumiana. Hivyo wanasheria wa kata wawepo hata wa ngazi ya diploma.

HITIMISHO
Kata ni chanzo kikubwa cha mapato nchini, kata zinakusanya mabilioni ya fedha yanayopelekwa serikali kuu Ili kupangiwa matumizi kwajili ya nchi. Hivyo serikali iwajali watu hawa wanaosaidia kwa asilimia kubwa sana kukuza kipato cha nchi. Kama serikali inavyothamini watumishi wa serikali kuu na ngazi za mikoa, basi vivyo hivyo iwathamini na watumishi wa kata, kufanya hivyo mapato yataongezeka mno na hatimae tuaifikia nchi ya ahadi Tanzania tuiotayo na tuitakayo.
 
Upvote 2
erikali kupitia Wizara zinazoajiri zipange bajeti ya kununua vifaa, kama vile simu, pikipiki na kompyuta mpakato, kwajili ya watumishi wa kata, ambavyo ikiwa mtumishi atapangiwa kwenye kata lazima akabidhiwe hivyo. Namba ya watu watakao ajiriwa itokane na vifaa vilivyotengwa kwa kipindi husika.
Watendakazi lazima wapatiwe vitendea kazi stahiki....... ni kosa na kinyume na haki kutoa kazi tu paai na vitendea kazi.

Ni kama kulazimisha mgonjwa afanyiwe operesheni na daktari bila kuweka mikasi na viwembe.
 
Back
Top Bottom