Utumishi wamepwaya kwenye utendaji kazi yao lini maboresho yatafanyika?

Utumishi wamepwaya kwenye utendaji kazi yao lini maboresho yatafanyika?

imekuaje

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
221
Reaction score
426
Habari.

Kwa kinachoendelea hakiitaji maelezo mengi sekretarieti ya ajira (PSRS) wamekuwa dhaifu na wamelewa.

Mpaka leo kilio cha wasaka ajira kupitia utumishi ni kile kile.

1.Kuchelewa kuita watu makazini kitu ambacho wao usema ni michakato sidhani kama ni lugha nzuri kwa sasa imezoeleka kutoka kufanya oral mpaka kuitwa kazini Mara zote imekua miezi 2 hadi 6 baada ya usaili.

2.Matangazo ya ajira yameongezeka zaidi kwa upande wa Halmashauri tofauti na miaka ya zamani tuliziona taasisi nyingi zikitoa matangazo ya ajira.

3.Kuchelewa kuita watu kwa usaili imekuwa kawaida mtu akiomba kazi kuanzia miezi 2 hadi mwaka ndipo wanaitisha usaili huu kwangu mimi naita Udhaifu na si mchakato.

4.Database (Kazidata) imekuwa yenye kurundika watu na kushindwa kuimaliza kwa wakati na mwisho wa siku inawabidi kuita watu kazini zaidi ya mwaka kama walivyofanya kwenye mikeka ya kuanzia mwezi wa sita mwaka huu au mwisho kutoka Matangazo mapya ya ajira.

Kwa Hali iliyofikia Utumishi imekuwa ni dhaifu na isiyo na DIRA tena kwa wasaka ajira.

Inatakiwa Transformation kubwa ifanyike ya.

1. Kuita watu usaili ndani ya mwezi mmoja Hadi miwili.

2. Kuita watu kazini kwa wakati mwezi mmoja Hadi miezi miwili.

Nje na Hapo kuna jipu linatengenezwa tutakuja kuliona miaka ya baadae.
 
Watajua Hawajui,walimu laki 2 nafasi elfu 2 wanaitisha usaili.
Uvccm wameisha
 
Psrs wanafanya uhuni kama uhuni mwingine,,
 
Mwanamke anaweza kubeba ujauzito hadi akajifungua bado tu hujapata ajira uliyoomba kupitia utumishi, sababu ukiuliza unajibiwa kuwa ni mchakato wa ajira. Ki ukweli wanatutesa vijana.

Kuwe na ukomo, mfano
1.Ukiomba ajira ndani ya wiki 4 utaitwa kwenye usaili
2.Baada ya usaili ndani ya wiki 6 utaitwa kazini.

Walau vijana tunakuwa tunajua kuwa ndani ya miezi miwili na wiki mbili mchakato wa ajira unakuwa umekamilika. Lakini hizi uncertainty ya ukomo wa mchakato unaumiza sana vijana.

Binafsi nina RECEIVED ina miezi mitano sasa na bado sijaitwa kwenye usaili. Inafikirisha sana
 
Hivi mnafikiria mchakato ni rahisi kihivyo?au unafikiri wanatangaza kazi ya ajira moja tu?au unafikiri kazi moja waombaji ni 10?unataka wakitangaza leo wiki ijayo wawaite watu kwenye usaili?pia jua suala la kuita watu kazini ni suala linalohusisha taasisi zaidi ya moja,,je hazina wakisema subilia hatuna hela za mishahara?
 
1.Sasa kama auna pesa unatangazia nini ajira?
2. Sasa kama mchakato mgumu auwezi unakupalia ulikubalije kuufanya?
3.na kama unajua waombaji wengi kwa nini unakubali kuanzisha mchakato angali ujajipanga kukabiliana nao kwa uwingi wao?
Nb ukiona kazi imetangazwa utumishi kwa niaba ya taasisi inayoitaji wafanyakazi Huwa wao wamekamilisha taratibu zote hapo suala ni utumishi TU wawapelekee hao watu na si hivyo unavyosema wewe ucheleweshwaji kwa 100%unafanywa na utumishi si taasisi zinazoajiri.
 
Basi haujui kitu,,,nikupe somo kidogo,,,ukiona tangazo la taasisi na umeambiwa maombi yapelekwe kwenye taasisi husika jua hapo sekretarieti haihusiki,,,wao wanabaki kama waangalizi tu wa mchakato,,mambo mengine yote yanafanywa na taasisi husika
 
Soma vizuri maelezo yangu yaelewe ndio jibu sasa hizo hoja.
Unachojibu Mimi sijakiuliza.
×××××××××××××××××××××××××××××
Na hata ukitaka hiwe hivyo kwa taarifa Yako taasisi zinazoita wenyewe usaili mambo yao yanakimbia chap sana kuriko wakipewa full authority hao watu wa utumishi longo longo nyingi
 
Back
Top Bottom