Sina data za uhakika ila ni kwamba wanalipwa kwa viwango vya kimataifa ambavyo ni karibu dola kumi kwa saa sawa na Tsh. 10,000.00 !! Naomba mwenye hakika zaidi atupatie data.
Sawa sawa kabisa.
Gross salary siyo net salary - ni malipo ambayo hayajakatwa kodi na madai mengine na RN au Registered nurse ni mtu muhimu sana haspitalini. Nilipo bado natafuta data zaidi lakini kama yuko anayeweza kusaidia, JF ni tambarare.
Ninavyoelewa wachache ambao wamejaribu kufanya hivyo wamenyamazishwa ama kwa kutishiwa au kufukuzwa kazi. Hivyo wengi wanaogopa hata kukohoa - kwanza hata hizo sheria sidhani kama wanazijua.
Wana JF, ningekuwa na data za kuaminika ningezileta ila hapa nilipo imeniwia vigumu kufanya hivyo. Nawaomba wote wenye access na namna ya kuzipata kuhusu hii hospitali na nyingine zozote zile zinazowanyonya wananchi wazitoe. Ninavyojua ni kuwa kama mtu analazimika kufanya kazi zaidi masaa ya ziada yanayoruhusiwa kisheria, alipwe !!