UTUMWA HURU: Mawazo changamshi

guzman_

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2016
Posts
1,268
Reaction score
2,330
Hivi karibuni nimekuwa nikifuatilia sana yanayotokea huko Africa ya Kazikazini. Watu weusi hasa weusi kutoka kusini mwa jangwa la sahara wamekuwa wakiuzwa kama nyugu bila kujali ubinadamu wao..nn chanzo chake hasa? wamefuatwa na kukamatwa kwao? jibu walienda kwa ridhaa yao. nini kiliwasukuma? Hebu ungana nami The Guzman_
Ukweli ni kuwa pamoja na kuwa biashara ya utumwa wengi wameishia kuisoma kwenye vitabu na kuaminishwa kuwa ilitoweka na ilikuwa wakati huo mm binafsi sikuwahi amini hilo. Utumwa hauto kaa uishe na muathirika hapa ni mtu mweusi (Black Africans). Kwa tuliobahatika kukata mbuga ukienda uingereza, marekani, Ufaransa, Ujerumani, Serbia, Portugal Italy n.k tembea utembeavyo lazima ukutane na hasa wanawake wanaotumikishwa kingono na kunyanyashwa pasipo huruma (morden slavery). Niliyo ya shuhudia ni meng..... nchi kama philipines kwa wanaojua wadada wao wengi ndio wanaotumikishwa madanguloni nearly everywhere in this world except in Africa. Sio walienda wakakatwa wakafungwa minyororo mithiri ya babu zetu NO hii una sulender mwenyewe na kukubali kutumikiswa.
Na sasa tunashuhudia our real fellow brothers/sisters are sold just like a sheep..ukiangalia nini hasa kimewafanya wakimbilie huko..jibu ni moja HALI YA UCHUMI na kukosekana kwa mifumo mizuri ya kuwasaidia vijan. Inawezekanaje kijana atoke Ethiopia akimbilie ulaya kupitia libya na akakumbane na hayo maswaibu..jibu ni kukosa fursa za kiuchumi. Nimekuwa nikifuatilia vipindi vya BBC kuna wadada walitoka Nigeria na kurisk maisha yao kupitia jangwa la sahara kuingia ulaya walikamatwa wakateshwa na kuuzwa kama nyugu lakini bado wanamiminika kwenda huko. Ukisikia habari za wadada wandani wanavyo nyanyashwa huko Uarabuni huwezi kuwa mpole kamwe lakini daily dada zetu wanamiminika na kila siku wanaulizia fursa huko (pathetic).
Nirudi kwenye mada hii Morden slavery haihitaji kuwa na prophet kuitabiri watu watajiuza wenyewe wapate ridhiki. Kiasi kikubwa taasisi kubwa kama IMF na World Bank plus WTO are working towards that end. Taasisi hizi kubwa zimeundwa mahususi kudhoofisha nchi za Africa na Caribbean wabaki kuwa tegemezi ili kuleta uwiano wa duniani..maskini na tajiri. Kwa nini nasema hivyo, soma sera zote ni za kinyonyaji mpaka unashindwa kuelewa watu tuliowaweka madarakani wanajua haya mambo kweli (mind you in Africa if your smart enough wanakuondoa).
MAMBO MAKUBWA MATANO YANAYO ASHIRIA UTUMWA HUU KUTOISHA
  1. Nchi nyingi za kusini mwa jangwa la sahara ongezeko la watu ni kubwa sana hasa vijana ukilinganisha na nchi yoyote duniani na hamna juhudi zinazofanywa kuhakikisha tunacopy na hili ongezeko la watu.
  2. Elimu yetu hasa hii tunaita formal education hii haiwaandai watu kuwa wazalishaji bali waelewa wa mambo yasiyo na msingi.. ukijua kua karl peter alikuja TZ inakusaidia nini? why not invest heavily on TVET? upgrade our system, support and finance entrepreneurial youth, invest on agricultural provide them with best technologies, support our domestic market etc Tunategemea sera zinazoletwa na U.S.A kufufua uchumi TZ (Hakia nani).
  3. Political system in S.S Africa is at I.C.U waiting for death announcement. Hapa ndio shida na hii inachagizwa na hoja ya 1 na 2. Bara la africa ndilo lenye watu maskini na wasio na elimu kuliko yote na hii imekuwa kura tulufu kwa vyama vinavyoongoza kuendelea kubaki madarakani bila kufanya mambo ya msingi na badala yake kucheza na akili za maskini na wajinga.
  4. Hii inatokana na sisi wenyewe mifumo yetu ya ndani (internal institutions)...hatuaminiani kabisa. mtanzania akianzisha kiwanda cha kusindika machungwa utasikia kelele huko nje balozi mpaka mkuu wa mipaka watasema wewe fisadi..mtu ukiwa tajiri huwezi pewa uraisi eti umepata wapi fedha..kiufupi tumeathiriwa na mentality za kiujamaa na kimaskini kupindukia. kila mtu anamwona mwenzie kama adui wa maendeleo..mpinzani vs mtawala....baada ya kukaa mezani tuone nini cha kufanya kwa masrahi ya taifa na watu wake tunaanza kunyosheana vidole. ukienda benki leo wewe na mchina leo watamkopesha mchina wanakuacha wewe unasugua benchi (This is everywhere in Africa). Hapa ndio tutakaposhuhudia wimbi kubwa la vijana wanao amini katika weupe wakienda huko kutafuta maisha.
  5. Mwisho ila siyo kwa umhimu waafrica tumejiweka kama kundi la mwisho duniani. sisi ni wazee wa last options. mitumba sisi, mchele fake sisi, maziwa yaliexpire sis, simu bei chee sisi n.k and we are comfortable..ukianzisha kiwanda cha kutengeneza baiskeli/helikopta bongo utaambiwa huna patent right.
WITO: Bara la Africa wasiungane kwa pamoja watafute suruhu ya kudumu kuliko kuendelea kuchekeana na mchina anaye nyonya mali za bara hili na kuendelea kujiimalisha. Kama tunafikir kuendelea kulilia misaada yenye masharti magumu ni suruhu basi tujiandae kujiepeka huko utumwani.
Haya ni yangu machache kwa leo.
 
Mkuu umenena vyema sana.
Kuna mamtu yatakuja na hoja za kikoloni hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…