Utumwa wa akili au nini?

Utumwa wa akili au nini?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Huu mchoro kwy ukuta wa Shule ya Upili ya Ben Mkapa una maana gani, muktadha gani na mantiki gani kwa ustaarabu wa zama hizi. Je, siyo dhalili kwa utu wa binadamu hususan weusi?

Angepiga mzungu picha kwenda kuanika kwao kuonyesha jinsi tusivyofaa sote tungempigia makofi lakini nikipiga mimi picha au wewe atazuka mtu kuhoji kwanini umepiga picha wkt ule mchoro umewekwa pale kwa ajili ya umma (hata usipoupiga picha umma utauona tu na kuujadili hata kimoyomoyo).

Nadhani wakati umefika tuhariri na kudurusu historia yetu. Siyo kila kumbukumbu hata iliyo dhalili tunaienzi milele yote.

20221202_131848.jpg
 
Wewe tatizo Dini yako sio watu wa elimu hujui historia umekalia kucheza bao na kusali ovyo.
 
Mwarabu anahusika na matatizo ya Africa kama kielelezo kinavyoonesha hapo ukutani.
Mwarabu aliuza weusi ni kosa hilo je, mzungu aliyenunuwa naye si alitenda kosa? Mwarabu hakuwa na mashamba ya kulimisha watumwa ila mzungu.
 
Wewe tatizo Dini yako sio watu wa elimu hujui historia umekalia kucheza bao na kusali ovyo.
Ungemalizia "na kumiliki visima vya mafuta"

Ila tuna haja kweli ya kuenzi historia inayotuonyesha jinsi babu zetu walivyofanyishwa kazi ngumu za mauti na za kuwapunguzia thamani ya ubinadamu wao; kwa malipo ya tonge 7 za ugali na punje 3 za maharagwe?

Superiority of Eurocentric history over inferiority of Afrocentric history.
 
Back
Top Bottom