Utumwa wa dini ni tatizo kwa Waafrika

Utumwa wa dini ni tatizo kwa Waafrika

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Jumapili usiku wa sa mbili hivi nilikwenda Stand Kuu ya mabasi yaendayo na yatokayo mikoani na nje ya nchi pale Ubungo ili kumpokea mjomba wangu aliyekua anatokea Tabora. Nilipofika pale nikampigia simu akanambia wapo Kibamba

Kwakua nilikua nahisi uchovu na usingizi kwa mbaali, nikaamua kushuka garini nikatafute japo chai au kahawa nichangamke kidogo. Nilifika kwenye mgahawa mmoja uliokua unaendeshwa na wanawake watupu nikakaa kwenye meza moja na jamaa aliyekua amebeba begi lake mgongoni huku anakunywa maji

Muhudumu alinifata na baada ya kumuagiza aniletee chai akataka kuongea pia na yule jamaa tuliekaa nae meza moja. Hawakuelewana. Jamaa anaongea kiingereza tu tena kwa lafudhi niliyohisi ni ya ki Nigeria na dada yule pamoja na wenzake wote pale hawakumuelewa

Nikajaribu kutoa kamsaada kangu ka kiingereza cha chini ya mwembe kwa Ras Simba na yule bwana akaletewa chakula alichokua anakihitaji, na baada ya hapo tukawa tunapiga stori za hapa na pale. Aliniambia yeye ni raia wa Ghana na sio Nigeria kama nilivyokua nimedhania awali

Nilichogundua ni kwamba jamaa alikua ana mahesabu makali mno nadhani kutokana na budget na pia safari yake ilikua bado ndefu mana alikua anaenda Uganda kisha aelekee DRC. Kwa ukarimu wa Kitanzania nikaamua nimlipie bill ya chakula na kinywaji alichokunywa, na jamaa kwanza akashangaa na kisha alipoona namaanisha alinishukuru sana sana!

Baada ya dakika chache mjomba akanipigia kunambia kua ndio wanaingia Ubungo stand na mie ikabidi niagane na huyo rafiki yangu Mghana ili nisogee kwenye basi

Basi wakati tunapeana mikono kuagana jamaa akanishukuru tena na halafu akanambia ukarimu niliomfanyia utaukumbuka sana. Kisha kwa sauti ya chini akaniuliza wewe ni dini fulani?(akiitaja jina). Nilidhani lile swali halikua na maana nikalipotezea, lakini akaniuliza tena!

Nikamwambia I am a human being. Kwamba mimi ni binadamu na chochote nilichofanya kwake kama ni kizuri na kitafanya anithamini basi nimekifanya kutokana na ubinadamu wangu kwanza

Na kama nimefanya chochote chenye kasoro na yeye akanidharau kwa kosa hilo basi ajue nimefanya hivyo kwa kasoro zangu kama binaadamu na wala sikutumwa na imani yangu ya dini!

Nikamwambia wazungu wanatucheka sana watu weusi tunavyoumizana na hata kuuana kwa jina la dini huku tukiwa hatufati values zinazohubiriwa na hizo dini kama vile kusema ukweli na kuacha uongo, kuacha wizi na ufisadi na kutendeana haki

Jamaa aliona aibu sana kwa maneno yangu yale na tukawa tumeagana bila hata ya kupeana contacts.

Nadhani kuna shida sana kwenye hili la dini hasa kwetu sisi waafrika. Kwa jina la dini watu wanauana, wanadhulumiana na kutendena ukatiliwa kila aina
 
NAJARIBU KUUNGANISHA DOTS NASHINDWA KUPATA MAIN POINT.
Ngoja wachungaji na mashehe waje wajazie nyama
Suala ni kwamba, kwanini mtu aunganishe wema au ubaya anaofanyiwa na mtu na dini yake? Ina maana hizi dini ndio zinawatuma waumini wake kufanya mema na mabaya?

Kwa mfano nini ni kipimo cha jambo jema na nini ni kipimo cha jambo baya?

Kabda ya kuja kwa dini katika jamii za kiafrika watu walikua hawafanyiani ukarimu? Je kabda ya kuja kwa hizi dini zinaa ilikua inachukuliwa kama kitu kizuri na kisicho na tatizo katika jamii hizo? Wizi je?

Sasa kwanini kabda mtu hajataka kua rafiki yako kwanza ataka ajue imani yako ya kidini nadhani hili si sawa
 
Kwamba dini hiyo ilotajwa ndio inamioyo ya kusaidia watu au sjaelewa kaka
Itakua sijui nimeandikaje dada naona wtu wengi hajanielewa

Maana yangu ni kwamba, binadamu tunapofanyiana wema hua tunafanya hivyo kwa ajili ya imani zetu za dini au ubinadamu wetu kwanza?

Kwanini unapomfanyia mtu jambo fulani akunasibishe na dini fulani? Kwamba umemkiribu mtu chakula au kinywaji labda halafu akwambie kwa ulivofanya hivi wewe utakua ni dini fulani
 
Itakua sijui nimeandikaje dada naona wtu wengi hajanielewa

Maana yangu ni kwamba, binadamu tunapofanyiana wema hua tunafanya hivyo kwa ajili ya imani zetu za dini au ubinadamu wetu kwanza?

Kwanini unapomfanyia mtu jambo fulani akunasibishe na dini fulani? Kwamba umemkiribu mtu chakula au kinywaji labda halafu akwambie kwa ulivofanya hivi wewe utakua ni dini fulani
hapa nimekuelewa kaka
 
na hilo ndilo metaka kukwambia sjui kama hajambo usiniulize kwa nini
Unaona sasa unavonipiga pini? Sasa kwanini nisikuulize kama hajambo wakati wewe ndio umepewa dhamana ya kujua hali yake kama yeye alivyopewa dhmana ya kujua na kuangalia hali yako?

Nani wa kumuuliza unadhani dada?
 
Back
Top Bottom