Utumwa wa dini ni tatizo kwa Waafrika

hua najiuliza kama yule jamaa aliyeigiza kama yesu (brian) akija bongo atapiga pesa kiasi gan
 
NAJARIBU KUUNGANISHA DOTS NASHINDWA KUPATA MAIN POINT.
Ngoja wachungaji na mashehe waje wajazie nyama
Main point ni kuwa kwanini jamaa alimuuliza wewe ni dini fulani! (akaitaja) means dini inadetermine matendo yako, kitu ambacho jamaa alikikataa.......
 
Kiuhalisia Dini sio Mbaya ila watu hawajui namna ya kucope na dini, Hakuna uhakika kama dini fulani inampeleka mtu peponi au la na hakuna uhakika kama kuna pepo au la, ila lengo kubwa la dini ni kuleta mshikamano duniani na amani.. sasa waafrika tatizo letu kubwa dini tunaichukulia kwa Emotions Kubwa.. wanaamini kila kitu hutoka kwenye dini.. Ndipo tunapokosea!
 
Jumamosi iliyopita nilipata wasaa wa kuongea na baba mzazi kuhusu haya mambo ya imani, watu wameanza kufumbuka fikra na muda sio mrefu huu utumwa wa kidini utaondoka. Nakumbuka kauli yake wakati tukiongea alisema "Lengo kuu la kuletwa dini ni kufanya watu wa chini tutii mamlaka".
 


Kaka mkubwa umeshawahi kutambua umuhimu wa dini ?

Je ushawahi kujiuliza kielimu ni yapi malengo ya dini ?

Kaka unaposema wazungu wanawacheka,huu ni ujinga uliopea kabisa,inaonekana kwako wewe wazungu ndio kipimo cha ustaarabu na kuelimika,hali ya kuwa ukweli wa mambo ni kinyume ?

Na unaposema wazungu wana kucheka una maanisha wazungu gani na wanakucheka kwanini ?

Je unafikiri kila mwafrika ana yafanya hayo unayohisi kwayo wazungu wanawacheka ?

Hapa nakupa malengo ya dini japokuwa swali hili nimekuuliza hapo juu,na ninajua usingeweza kulijibu.

Malengo ya dini :

1. Dini imekuja kuilinda akili ya mtu

Hili ni miongoni mwa malengo ya dini,kuja kwake ni kuilinda akili ya binadamu isifisidike,yaani isiingiwe na uchafu na kuyakemea yote yapelekayo akili kuharibika,kama vile matumizi ya pombe,madawa ya kulevya na mfano wake.

2. Dini imekuja kulinda mali za mtu

Hili pia ni lengo la dini. Kuwepo kwa dini watu watajua kuchunga amana za watu,kuepuka dhuluma,kutafuta machumo ya halali,kuacha kula mali za mayatima na mfano wake.

3. Dini imekuja kulinda vizazi vys watu.

Hapa ndio maana unakuta dini inakemea sana uzinzi na mfano wake.

4. Dini imekuja kulinda na kichunga heshima ya mtu

Hapa dini imekuja kutufunza jinsi ya kuishi na wenzi wako,wapendwa wako na maadui zako na mfano wake.

5. Dini imekuja kututoa kutoka katika hali duni kiutendaji kwenda katika hali ya juu kiutendaji

Dini imekuja kurekebisha zile ada na desturi za kihayawani,ushirikina na ujings mwengine.

Narudi..........
 
Udini ni jambo baya sana,nani niliwahi kuulizwa dini yangu kisa MTU aliyegonga mbuzi wangu na gari,NIMEMSAMEHE. wakawa wanasemezana jamaa ana moyo sana atakuwa m....wanataja jina la dini,nilishangaa sana
 
Udini ni jambo baya sana,nani niliwahi kuulizwa dini yangu kisa MTU aliyegonga mbuzi wangu na gari,NIMEMSAMEHE. wakawa wanasemezana jamaa ana moyo sana atakuwa m....wanataja jina la dini,nilishangaa sana
Umenielewa sana mkuu, asante
 

Zurri asante sana kwa mchango wako kwenye hii mada. Bahati nzuri nakubaliana nawe kwa asilimia zote katika kile ulichoandika kuhusu mchngo wa dini kwa mwanaadamu

Nina maswali madogo machache tu kwako, kwamba kabda ya kuja dini za kitabu jamii zilikua hazina ustaarabu? watu walikua wanauana hovyo? Watu walikua wanazini au kufanya ngono hadharani? Watu walikua wanasema uongo? watu walikua wanadhulumiana?

Nikupe taarifa tu mkuu, Wamarekani na hata wazungu wengi sana sio wafatiliaji wa mambo ya dini hata kidogo na kuna wengi ambao hawajawahi hata kukanyaga tu kwenye nyumba za ibada mpaka wanaingia kaburuni

Lakini wazungu wana moral values zao ambazo mtoto anafundishwa tangia akiwa mdogo. Miongoni mwa hizo ni kusema ukweli.

Huku kwetu sisi waafrika pamoja na kua tumepokea na tuna practice hizo imani lakini uongo ndio asili yetu. Kiongozi wa dini kama Padri, Mchungaji, Shehe anaweza kua muongo wa mchana kweupee ndio mpigaji pesa kwa kutumia nyumba yake ya ibada

Sizungumzii waumini wa kawaida, nasemea viongozi wa dini kabisaa, baadhi yao wamewahi kuzaa na hata kufumaniwa na wake za watu, wengine wanaharibu watoto waliopewa na kuaminiwa na wazazi kuwalea kwa kuwalawiti, wengine ni walevi mbwa na hata mafisadi na wanaodhulumu watu pia wapo. Mambo haya unaweza usiyakute katika jamii zingine ambazo hazifati dini ila zinakua na strong human and moral values

Zipo shule za dini hapa nchini kwa mfano ambazo zinajulikana hua zinafanya vitendo vya ku cheat mitihani ili wanafunzi wake wafaulu na matokeo yake kutuletea madaktari na ma injinia incompetent! Hapa mchango wa dini uko wapi?

Toka enzi na enzi hadi sasa hivi tunavyoandika humu JF binaadamu amemwaga damu nyiingi sana kwa jina la dini! Rejea mauaji ya kugombea madaraka miaka kadhaa baada ya kufa kwa Mtume Muhammad SAW, rejea vita ya msalaba (Crusade) ya kuisafisha Ulaya na athari za uislamu, rejea damu inayomwagika Yemen na kwingineko ambapo katika karne hii ya 21 watu wangekua wameamka!

Ninaposema wazungu wanatucheka ni kwamba wao hawafuati hizo dini lakini hawauani, hawadhulumiani, hawasemi uongo na wanatendeana haki. Huku kwetu wanatuuzia silaha halafu wanatuchonganisha kwa imani zetu za kidini na kwa uzuzu wetu tunaanza kuchinjana! Kwanini sasa wasitucheke?

Nilipomlipia chakula yule Mghana tuliekutana pale Ubungo Bus Terminal nilifanya hivyo kwa msukumo wa ukarimu wa kibinaadamu na wala sikutaka kujua yeye ni wa imani gani. Yeye sasa akataka kunasibisha takrima ile na imani yangu ya dini

Mimi nina imani yangu ya dini lakini nilishangaa yeye kutaka kuunga tukio lile na imani ya dini. Inamaana kama angeibiwa pia angefanya hivyo! Na hapa ndio nikamwambia wazungu wanatucheka kwa mambo hayo
 


Waafrika ni watumwa wa dini ambazo kiualisia hazituhusu hata kidogo, tumeletewa tu kupotoshwa na kuchezewa akili kama ilivyo sasa. Na uzuri usiopingika ni kwamba ukifuata sana hizi dini za kuletewa (uislam na ukristo) mwishowe LAZIMA tu utakuwa mnafiki. Yaani hizi dini imekuwa kama laana kwetu na nahisi hata miungu na Mungu wetu anatushangaa kwanini tumeacha mila na Imani zetu kufuata Imani za watu zisizotuhusu. Inasikitisha kwa kweli. Imagine mwafrika mweusi unajiita jina la kiyaudi au la kiarab, huu si ujinga jamani? Hivi kuna myaudi ama mwarab yeyote aitwaye jina la kiafrika anyooshe kidole tumuone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…