Kgy26
Member
- Sep 14, 2022
- 6
- 4
Afya
Afya ni hali ya kuwa na ustawi au kujisikia katika hali nzuri kimwili, kiroho, kiakili na kijamii.
WHO inabainisha kuwa afya ni kuwa na ustawi kimwili, kiakili na kijamii.
Aina za Afya
Afya ya kiakili, inajumuisha hisia, tabia na mitazamo ya mtu kuhusu binadamu wenzake na jamii kwa ujumla. Ni mwenendo wa mtu anavyo jiona, uhuru na ustawi binafsi vinashawishi katika afya ya akili ambavyo hupelekea wasiwasi, uoga, mawazo na hata kurukwa na akili.
Afya ya Mwili na uzazi hii inahusika mfumo wa mwili na viungo vya mwili. Afya ya uzazi inahusika na ufanisi wa mfumo wa uzazi na viungo vya uzazi.
Afya ya binadamu inaweza kuwa nzuri au kudhoofu kutokana na sababu zifuatazo;
· Biologia au maumbile ya binadamu, kutokana na sababu za magonjwa ya kurithi au hitilafu katika utungaji, ukuaji na uzazi wa mtoto yanaweza kuathiri afya ya binadamu
· Mazingira, Sababu za uchafuzi wa mazingira nafasi ya mwili au miundo kama nyumbani, mahali pa kazi, maeneo ya umma na pia sababu za kijamii na kitamaduni vinaathiri moja kwa moja afya ya binadamu.
· Mtindo wa Maisha, namna binadamu anavyo jiweka katika masuala ya usafi, ulaji (lishe bora), tabia binafsi, mazoezi ya mwili, mahusiano kijamii na shughuli za ngono vina athari katika afya ya binadamu.
· Ongezeko la sumu mwilini ni chanzo cha magonjwa, sumu huingia mwilini kwa kupitia, madawa ya hospitalini, vyakula vilivyolimwa kwa mbolea za viwandani, kemikali za kutunza mazao, nyama za mifugo ya kisasa, vyakula vya papo kwa papo (Fast food), vyakula vya kusindika kutoka viwandani, vipodozi na dawa zenye kemikali, pombe na sigara, moshi wa magari na wa viwandani, viyoyozi ofisini, njia za uzazi wa mpango wa kisasa.
· Uzito na unene uliopitiliza ni chanzo cha magonjwa mengi, unatokana na ulaji uliopitiliza wa chakula aina wanga na sukari, ambavyo huzalisha nishati mwilini, na ikizalishwa nyingi kuliko inayohitajika uhifadhiwa kama mafuta mwilini na kusababisha unene uliopitiliza, madhara ya unene uliopitiliza kisukari, ugonjwa wa moyo, vifo vya ghafla, kansa za aina mbali mbali, kuishiwa nguvu za kiume, ugumba kwa wanawake, mvurugiko wa hormone, magonjwa ya joint, presha za damu, kukosa usingizi, kupooza au kiharusi.
Hata hivyo kwa nchi ya Tanzania athari za kiafya hutokana na sababu nyingi mfano
KIMWILI NA KIUZAZI
kushindwa kupima afya mara kwa mara, kujinunulia madawa unapohisi ni ugonjwa fulani, utamaduni wa ngoma za kiasili zinachochea ngono zisizo salama, kipato cha chini kiasi cha kushindwa Kwenda hospitali mtu ajisikiapo kuumwa, kuacha au kuongeza dozi, kutafuta tiba mbadala badala ya hospitali.
Unyanyasaji wa kijinsia kama ukeketaji, ubakaji na kulawitiwa, kukosa matibabu sahihi wakati wa hatua ya uleaji wa mimba hadi kujifungua, ukosefu wa kipato kufuatilia afya ya uzazi, ukosefu wa mlo kamili, changamoto katika mfumo wa hormones, ngono zembe na athari za dawa na kemikali zinazoathiri mfumo wa uzazi kama mekyuli migodini huathiri nguvu za kiume
KIAKILI
Kuumizwa kimapenzi kuachwa, kuachika, kufiwa, kufumania, kuwa tegemezi na kushindwa kuhudumia, kuwa na majukumu mengi na kuwekwa katika presha ya kuyakamilisha, kukosa tumaini la maisha kwa kuona hali ni magumu kiuchumi, fikra hasi juu ya uhalisia wa maisha.
Ili kukwepa madhara yoyote yanayojitokeza kutokana na kukosa afya bora hatuna budi kufanya yafuatayo;
- Kuweka utaratibu wa kula vizuri, kula mlo kamili kwa kiasi kinacho takiwa na muda unaotakiwa. Mwongozo sahihi wa namna ya kula ( balanced diet plan) unaelekeza kuacha kula kwa kiwango kikubwa chakula aina ya wanga na kutopata virutubisho kamili ambavyo mwili unahitaji, ili kuweza kupungua na kubaki na uzito salama ni lazima kujenga tabia ya kula mlo kamili na kuepuka kula vyakula vya viwandani ambavyo vingi vina sukari, mafuta na wanga mwingi zaidi ya mahitaji ya mwili, pia ni vizuri kujua mwili wako unahitaji kiasi gani cha wanga kulingana na umri wako, kazi zako, jinsia yako, Uzito wako na urefu wako.
- Kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini (Cleansing and detoxification programs), mwili una huwa uchafu mwingi kwenye mfumo wa chakula na Kama mwili una ongezeko Kubwa la sumu, basi mwili utalazimika kuyang'ang'ania mafuta ili kuzilinda ogani zake muhimu dhidi ya sumu kusababisha mafuta mengi kubaki sehemu za tumboni kuzunguka ogani zisizulike pia kwenye mishipa ya damu. Ili kuruhusu mwili uachie mafuta ni lazima Kwanza kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini kuondokana na utumwa wa unene uliopitiliza.
- Mwongozo sahihi wa namna ya kufanya mazoezi(physical exercise programs) lazima kujua kwamba kufanya mazoezi sio tu kwa ajili ya kupungua uzito bali ni jambo la msingi ili kuwa na Afya njema, usipoushughulisha mwili wako, misuli yako ya mwili inawahi kuchoka hivyo inapelekea mwili kushindwa kutumia chakula cha wanga na mafuta kuzalisha nguvu na kupelekwa mrundikano wa mafuta yanayo leta Unene Uliopitiliza. kufanya mazoezi mara kwa mara inasaidia asilimia 10 % ya utimamu wa mwili kusaidia mwili kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na hata mmeng'enyo wa chakula na mapigo ya moyo kukaa sawa.
- Kuhifadhi mazingira yetu kuzuia magonjwa ya milipuko, uchafuzi wa mazingira hata uwepo wa viumbe hatari kwa afya kama nyoka, tandu, inzi , mbu, mende na kunguni. Pia mazingira yakiwa mabaya huchochea msongo wa mawazo na kukosa utulivu.
- Kuwa na tabia njema kuacha hasira, ngono, ugomvi, wizi, kinyongo, chuki, kusamehe na tabia nyingine kama hizi hii itasaidia afya ya mwili na ya akili kwa maana itapunguza kasi ya mwili kufanya kufanya kazi kwa utaratibu sahihi.
- Kufikiri chanya kuhusu uhalisia wa maisha, namna maisha yakiangaliwa kutokana na matukio kama ajali, ukosefu wa ajira, rushwa, wizi, mauaji na mengine kama hayo,kwa jicho la kawaida pasipo kujua vyanzo vya matukio hayo anaweza kuchukulia kana kwamba dunia ni chungu na sio sehemu salama ya kuishi na kuibua sintofahamu na mawazo bila kutambua kuwa kuna fursa katika changamoto hizo ni binadamu anapaswa kuzitatua.
Mwisho
Afya ni mtaji, ili kufanya kazi unahitaji kuwa na afya kamili kiroho, kimwili na kiakili. Kuwa na afya ni uchaguzi binafsi na uamuzi wa kutendea kazi taratibu kamili za kuwa na afya husika mfano kuimarisha afya ya roho ni kumrudia muumba na kufuata mafundisho ya kiimani yatakayoimarisha roho pasipo wasiwasi, kimwili kula mlo kamili, kufanya mazoezi na kujikinga na athari za mazingira na kiakili kusikiliza, kutazama,kusoma na kutafakari mambo ambayo yanaimarisha akili.

Upvote
3