achengula
JF-Expert Member
- Jul 30, 2009
- 369
- 62
Bwawa la samaki linahitaji matunzo ya mara kwa mara ili kuhakikisha linakaa katika hali inayostahili kuwawezesha samaki kuzailiana au kustawi vizuri. Bwawa lisipopewa matunzo mazuri linaweza pelekea wadudu wa magonjwa kujitokeza na kukuletea hasara kubwa sana katika ufugaji wako. Tafsiri ya wafugaji wengi wa samaki ni kwamba ukishatengeneza bwawa basi kinachofuata ni manufaa ya haraka na bwawa litadumu milele bila hata ya kulifanyia matengenezo madogo madogo. Dhana hii ni potofu wala hakuna ukweli wowote, bwawa linahitaji uangalizi wa karibu sana ili kama kuna tatizo lililojitokeza liweze kurekebishwa kwa wakati. Bwawa linaweza kubomoka kingo zake, kuvujisha maji, kujaa matope au kuota miti ndani.
Hakikisha unaliangalia bwawa lako kwa kina ili kubaini kama kuna matatizo kwenye bwawa lako. Fanya marekebisho mara moja unapoyabaini ili kulifanya liendelee kuwa katika hali ya ubora na kulifanya lidumu kwa muda mrefu.
Mambo muhimu ya kuangalia kwenye bwawa soma hapa SEKTA YA MIFUGO TANZANIA