Utunzaji wa magari

Utunzaji wa magari

Msolopaganz

Member
Joined
Jan 16, 2019
Posts
25
Reaction score
36
Habari zeni wana JF, kuna hili swala la utunzaji wa magari kwenye mazingira yetu ya africa yanachangamoto sana. Gari used linakufikia toka japan au Europe unakuta halijawahi kukanyaga chini hatakama limekanyaga nimalachache sana.

Baada ya miaka miwili toka linunuliwe unakuta gari limezeeka. Achilia mbali wale wanaofuga gari, gari mwezi halijatoka nje ya geti.

Unaweza kua ni mtunzaji mzuri sana,unalifatilia gari yako katika kila nyanja bado tunafeli. Baadhi ya maeneo yanayotuangusha katika utunzaji wa ndinga zetu ni kama yafuatayo:

1. Umepaki gari nyumbani nje ya geti ili uingie ndani ujiandae na mishemishe, unatoa unakuta watoto wa kitaa washalichora bonge la mstari.

2. Gari ipo ndani ya geti unavitoto ndo vinajifunza kuandika, unakuta gari limecholwa numbers na makatuni.

3. Umepaki gari pembezoni mwa barabara unarudi unakuta bodaboda wamelikwaruza.

4. Umelipeleka car wash jamaa kitambaa katoka kuoshea mabampa au kilidondoka anakiokota anakipitisha kwenye body, mwishowasiku unakuta mikwaruzo midogo midogo.

5. Barabara zetu nazo changamoto, kutwa gari linapita kwenye madimbwi ya maji na makorongo hasa njia za mitaani. Kunasiku nilikua naelekea mwanza nilikanyaga shimo kwenye lile eneo baada ya kibao cha karibu mwanza nikiwa na speed ya 140k/h nilipinda rim na nikaua shockup, ilikua mwaka jana sasahivi wameweka viraka.

6. Garage zetu nazo kibongo bongo changamoto. Fundi kashindwa kuludishia kifaa anakwambia hiki chamzungu hakina kazi kinaachwa sababu tu kakifungua kashindwa kukirudishia.

7. Mbwa na makuku ya kienyeji pale home nayo balaa.

Ogeza na zakwako.
 
Kuna jamaa yangu wakati gariyake haina ata mwezi alinunua kuku wa kienyeji kwaajiri ya kitoweo, yule kuku wakamuachia ajitafutie chakula mule getini. Keshoyake akaniambia yule kuku aliliparua lile gari namakucha yake wakati akipigana na kinvuli chake. Asubuhiyake alimchinja, gari mpya ikawa na mikwaruzo.
 
Unapishana na marori na Magari mengine rough road vioo vyote unashusha vumbi linajaa ndani balaa! Kibaya zaidi ndio desturi yako! Baada ya muda kidogo tu Gari linakuwa kama lakufugia bata, kitimoto, n.k
 
Habari zeni wana JF, kuna hili swala la utunzaji wa magari kwenye mazingira yetu ya africa yanachangamoto sana. Gari used linakufikia toka japan au Europe unakuta halijawahi kukanyaga chini hatakama limekanyaga nimalachache sana.

Baada ya miaka miwili toka linunuliwe unakuta gari limezeeka. Achilia mbali wale wanaofuga gari, gari mwezi halijatoka nje ya geti.

Unaweza kua ni mtunzaji mzuri sana,unalifatilia gari yako katika kila nyanja bado tunafeli. Baadhi ya maeneo yanayotuangusha katika utunzaji wa ndinga zetu ni kama yafuatayo:

1. Umepaki gari nyumbani nje ya geti ili uingie ndani ujiandae na mishemishe, unatoa unakuta watoto wa kitaa washalichora bonge la mstari.

2. Gari ipo ndani ya geti unavitoto ndo vinajifunza kuandika, unakuta gari limecholwa numbers na makatuni.

3. Umepaki gari pembezoni mwa barabara unarudi unakuta bodaboda wamelikwaruza.

4. Umelipeleka car wash jamaa kitambaa katoka kuoshea mabampa au kilidondoka anakiokota anakipitisha kwenye body, mwishowasiku unakuta mikwaruzo midogo midogo.

5. Barabara zetu nazo changamoto, kutwa gari linapita kwenye madimbwi ya maji na makorongo hasa njia za mitaani. Kunasiku nilikua naelekea mwanza nilikanyaga shimo kwenye lile eneo baada ya kibao cha karibu mwanza nikiwa na speed ya 140k/h nilipinda rim na nikaua shockup, ilikua mwaka jana sasahivi wameweka viraka.

6. Garage zetu nazo kibongo bongo changamoto. Fundi kashindwa kuludishia kifaa anakwambia hiki chamzungu hakina kazi kinaachwa sababu tu kakifungua kashindwa kukirudishia.

7. Mbwa na makuku ya kienyeji pale home nayo balaa.

Ogeza na zakwako.
Umedadavua vizuri, jamani mi yale madimbwi ya ile mimaji michafu full kuua bushings

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna rafiki yangu alipaki gari jamaa akaja akawa amejiegemeza akaegemea window spoiler ikavunjika......kuna kero kama hizi unapaki gari watu wanafanya kitu cha kujiegemeza....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapishana na marori na Magari mengine rough road vioo vyote unashusha vumbi linajaa ndani balaa! Kibaya zaidi ndio desturi yako! Baada ya muda kidogo tu Gari linakuwa kama lakufugia bata, kitimoto, n.k
Kwanini ushushe vioo chini kwenye barabara yenye vumbi? na huku gari ikitoka japan AC yake inakuwa kali kama mpya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom