briophyta plantae
Senior Member
- Feb 18, 2017
- 117
- 132
Utunzaji wa mazingira na maliasili zetu kwa kizazi kijacho.
Serikali kwa ujumla imekuwa ikiweka mikakati mbali mbali na uundwaji wa sera zitakazowezesha utunzaji wa mazingira na maliasili tulizonazo na kwa hakika wana mipango na sera nzuri japo changamoto kubwa ikionekana kuwa ni utekelezaji,pia watika mwingine kukosa mbinu mpya na mbadala wa zile zilizoshindwa kutekelezeka.
Moja ya mapendekezo niliyonayo ni kutumia rasilimali watu katika jamii kurahisisha utekelezaji wa baadhi ya mipango. Kuna watu katika makundi mbalimbali wanaopatikana katika jamii, mfano wanafunzi, wakulima, wana michezo n.k. wanaoweza kutumika kwa kuwezeshwa na kupewa elimu katika masuala ya mazingira na wakafanya mabadiliko makubwa.
Siyo ngumu serikali kufanya kazi ya uzalishaji miche ya miti kwa wingi na shughulia ya upandaji na utunzwaji kuachwa kwa jamii hizi zilizo katika makundi ili kurudisha mazingira yaliyokuwa yameharibiwa kwa ukataji miti holela pamoja na ufugaji usio na utaratibu.
Mfano 'kila mwanafunzi wa shule kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa la saba kwa shule za msingi akapewa miche mitano tu ya panda na kuitunza katika mazingira yanayomzunguka iwe ni shuleni hapo hapo, nyumbani ama kwenye maeneo maalumu watakayopangiwa kwa kila mwaka anapokuwa shuleni iwe ni moja ya stadi zake za kazi katika masomo', hadi huyo mtoto mmoja anamaliza darasa la saba atakuwa amepanda miti 35.
Je, hapo itategemea na wastani wa shule ina watoto wangapi na kila mwaka wanaingia wangapi,ndani ya miaka kadhaa mbele tutakuwa tumerudisha katika hali yake maeneo mengi sana yaliyoharibiwa kwa ukataji miti holela.
Tukija katika suala la taka taka, utekelezaji ungeanzia kwa uwajibishaji kwa watu wanaoshindwa kuzingatia swala la usafi wa mazingira na afya ya jamii inayomzunguka kwa kutokudhibiti uzalishwaji wa taka na utunzwaji wake mpaka kufikishwa maeneo maalum yaliyotengwa.
Kuna ma bwana afya na mabibi afya katika kila kata ila usimamizi na uwajibishaji umekuwa changamoto kwakweli. Na kwa sehemu kubwa serikali kwa kushindwa kutenga maeneo na utaratibu mzuri wa ukusanyaji wa taka imekuwa ikichangia mazingira kuharibika sana na hii inawapa watu sababu kubwa ya kujitetea.
Pili ili kuweza kutekeleza mipango iliyopo kwa urahisi basi serekali inatakiwa kuhakikisha wananchi hawapati sababu bali wanapaswa kuwajibika.
Kutengwe maeneo maalum ya kutupa na kuhifadhi taka kwa kila kata.
Kuwe na gari, mkokoteni wa kuvutwa na binadamu ama mnyama kwa kila kata ili kurahisishwa ukusanyaji wa taka.
Kila mwananchi kuwa mlizi wa mwenzake na uwajibishwaji katika ulipaji faini uzingatiwe kikamilifu bila woga wala kuoneana haya. (sioni kama ni tatizo mtu akimkamata mwezake akiharibu mazingira na kumtolea taarifa kulipwa asilimia 30 ama 40 ya faini atakayopigwa mtu aliyefanya kosa la kuchafua na kuharibu mazingira, vijana hawana kazi, hapo kila mtu atamchunga mwenzake, ni fursa kwa watu hiyo katika kutunza mazingira)
Kwa kufatisha haya ndani ya miaka mitano ama kumi tutakuwa na TANZANIA yenye mazingira yaliyobora sana kwa binadamu na wanyama.

Upvote
6