Utunzaji wa miguu hasa kwa wale ambao miguu hupasuka

Utunzaji wa miguu hasa kwa wale ambao miguu hupasuka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
  • Loweka miguu inayopasuka kwenye maji ya uvuguvugu na yaliyoongezewa sabuni
  • Kisha loweka miguu kwa muda wa dakika 10 hadi 15 hivi kwenye mchanganyiko wa asali kikombe kimoja ndani ya galoni moja ya maji. Hii husaidia kuondoa ngozi iliyokufa na kuzuia damu kutoka katika mipasuko.
  • Sugua miguu kila siku kwa jiwe laini ambalo halikwangui sana.
  • Kausha miguu vizuri kwa taulo au kitambaa cha pamba hasa katikati ya vidole vya miguuni ili kuzuia kuvu na bakteria kuzaliana kwa urahisi miguuni.
  • Paka mafuta, cream ya miguu au lotion yenye virutubisho kama vitamin E, siagi au Aloevera. Mafuta ya nazi au parachichi pia yanaweza kutumiwa kulainisha miguu. Vipodozi hivi vinaweza kutumiwa mara 2, asubuhi na jioni kila siku.
  • Usitumie wembe au kisu kuondoa mipasuko hii. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha mipasuko na madhara zaidi.
  • Vaa soksi kila siku unapokwenda kulala wakati wa usiku. Msichana unaweza kuvaa soksi nyeupe kwa ajili ya kuzuia vumbi lisiingie ndani ya mipasuko ya miguu. Soksi nyeupe ni nzuri kwa vile hazitunzi joto jingi na kusababisha unyevunyevu miguuni.
  • Dhibiti magonjwa au hali zinazochangia miguu kupasuka kama vile kukauka kwa ngozi (Xerosis); kuwa na uzito mkubwa, kusimama kwa muda mrefu, magonjwa ya ngozi kama vile mzio wa ngozi (Psoriasis na Eczema), ugonjwa wa kisukari na utendaji wa chini ya kiwango wa tezi la shingo.
 
Back
Top Bottom