Utunzi: Sauti ya mnyonge

Utunzi: Sauti ya mnyonge

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
893
Reaction score
1,021
Pesa si matumaini yao

Ni msukuma mkokoteni
Tena na jua kali kichwani
Pato lake sio ahueni
Pesa si matumaini yao

Ajabu mwajiriwa tajiri
Na mwajiri wake ni fakiri
Analipa, kipato swaghiri
Pesa si matumaini yao

Nao wakulima mashambani
Na wakulima wabaharini
Uhai wao uhatarini
Pesa si matumaini yao

Nao wabeba zege vichwani
Wabeba magunia begani
Bado kula yao tafarani
Pesa si matumaini yao

Nao huomba wasiugue
Ili pochi zao zipumue
Lizame jua wajizimue
Pesa si matumaini yao

Na wapo tayari kwa lolote
Washa jitoa kwa mambo yote
Hawaogopi kitu chochote
Pesa si matumaini yao

Ufukara si chaguo lao
Japo ndo hasa maisha yao
Ni kidogo sana pato lao
Shida ni mkate wa kesho tu
Hadi Mola akiwachukua
Pesa si matumaini yao

Abuuabdillah ✍️🇹🇿
0718569091
Credit Wasakatonge
 
Back
Top Bottom