Uturuki yaongeza mishahara ya wafanyakazi wa umma kwa 45%

Uturuki yaongeza mishahara ya wafanyakazi wa umma kwa 45%

Exile

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2021
Posts
1,477
Reaction score
3,642
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameangaza nyongeza ya asilimia 45 ya mshahara kwa wafanyikazi wa umma 700,000 siku tano kabla ya uchaguzi mkuu.

Haya yanajiri wakati uchumi wa nchi hiyo ukiyumba kutokana na athari za matetemeko makubwa ya ardhi mwezi Februari.

Erdogan, ambaye alichaguliwa kuwa rais wa Uturuki mwaka 2014, atawania muhula mwingine katika uchaguzi wa rais na wabunge mnamo Mei 14.

Kura za maoni zinaonyesha Erdogan anakabiliwa na kinyang'anyiro kikali kutoka mgombea urais wa upinzani, Kemal Kilicdaroglu.

Uchumi wa Uturuki ni suala muhimu kuelekea uchaguzi wa Jumapili.

Hatua ya Erdogan ya kupunguza kwa viwango vya riba kusiko kwa kawaida kulisababisha kushuka kwa thamani ya lira ya Uturuki mwishoni mwa 2021 na kufanya mfumuko wa bei kufikia asilimia 85.5 mwaka jana, kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa ndani ya miaka 24.

NB: ukiachana na mambo ya kisiasa, nchi hiyo kukumbwa na tetemeko ila inawajali wafanyakazi kwa Tanzania tungeweza.

Source: BBC swahili
 
Hii ni sawa na rushwa, aboreshe huduma za kijamii na usalama wao na mali zao na ilibid afanye haya kabla ya uchaguzi.
 
Alafu akishashinda uchaguzi inatokea inflation 101% wananchi wanaambiwa sababu ni uviko 19 😃
 
Back
Top Bottom