Uturuki yarudisha raia wake nyumbani kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania kutokana na maambukizi ya Corona

Uturuki yarudisha raia wake nyumbani kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania kutokana na maambukizi ya Corona

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Raia wa Uturuki wamehamishwa kutoka Ujerumani na Tanzania mapema Jumapili na kuwekwa chini ya kizuizi(karantin) cha siku 14 ili kupunguza kuenea kwa virusi vya corona.

Jumla ya Waturuki 157 kutoka Ujerumani wamepelekwa mkoa wa Kayseri na baadaye kupelekwa katika mabweni ya wanafunzi kwa ajili ya karantini baada ya ukaguzi wa kiafya.

Halikadhalika, Uturuki imewarudisha raia 53 kutoka Tanzania, Walifika Ankara kwa safari ya ndege na walipelekwa Kirikkale kufuatia taratibu kama zilizowekwa mjini Kayseri.

Uturuki imerudisha karibu watu 70,000 kutoka mataifa 107, chini ya maagizo ya Rais Recep Tayyip Erdoğan na kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya nje.

Ankara iliripoti kesi 148,067 za virusi vya corona siku ya Jumamosi, huku watu 108,137 wakiwa wamepona kabisa. Idadi ya vifo imefikia 4,096.

Zaidi ya kesi milioni 4.63 zimeripotiwa katika nchi 188 tangu virusi hivyo kutokea nchini Uchina Desemba mwaka jana, na maeneo yalioathirika zaidi yakiwa Marekani na Ulaya.

Sehemu kubwa ya wagonjwa wa COVID-19, karibu milioni 2, wamepona, lakini virusi hivyo vimechukua zaidi ya maisha 311,000, kulingana na data iliyokusanywa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha Marekani.
 
Wamesikia maneno ya wapiga ramli dhridi ya Tanzania bila kujua hizo ni propaganda za kuwaaminisha watu wao kwamba wao wako vizluri kulilko sisi hivyo wakubali kufungiwa ndani.

"Akili ya kuambiwa ongeza na ya kwako" ( Kwa Sauti Mh. Mzee Kikwete)
 
Kwahiyooo uturuki wajawapima watu wao kutoka bongo na kuwakuta wote wana c19? Wawaache watawauwa hukoo waombe vipomo kutoka Kenya ili wakiwapima kutoka tz wagundulike wanao, si unajua machine zinatofautiana kulingana na nchi hivyo vya Kenya ni vizuri dunia nzima na havidanganyi juu ya watu kutoka tz
 
Jumamosi nimeona basi kibao za mjenzi wa SGR zinarudi Dar huku zimejaa Waturuki, sijui ndio ilikuwa safari ya kurudi kwao?
 
Back
Top Bottom