Chifu Songea
Member
- Sep 9, 2024
- 30
- 46
Moyo wangu umeguswa kuwapongeza Azam Tv kupitia channel yao ya UTV kwa habari zao motomoto na za kina, zilizosheheni uchambuzi wa kiuweledi na kitaaluma. Hongereni sana na endeleeni kutuhabarisha watanzania na walimwengu kwa ujumla. Pamoja na pongezi hizo, ipo kasoro moja ambayo mmedumu nayo kwa muda mrefu sasa, nisijue kuwa huwa hamuioni ili mjirekebishe, au hakuna wanaowaambia juu ya kasoro hiyo? Au pengine ni makosa ya kiufundi??? Hii huwa naiona mara nyingi sana wakati wa taarifa zenu za habari. Ambapo huwa mnachanganya sana majina ya watu kwenye habari zenu. Mathalani, mtu anatokea kwenye habari, akiwa anajulikana kabisa kuwa huyu ni Dkt. Elisha Osati, lakini nyinyi mtampachika jina jingine kabisa, unaweza kukuta mmempa jina la Esther Bulaya. Hii naiona mara nyingi mno kwa kuwa napenda kufuatilia habari zenu. Sasa najiuliza tatizo huwa liko wapi??? Na ikitokea hivyo huwa hamrudi hata kufanya marekebisho. Kwa hilo, UTV limeshushia credibility!