UUGUZI KADA MUHIMU
Uuguzi ni moja ya fani muhimu katika sekta ya afya. Ni kada inayohusiana na huduma kwa ukaribu Zaidi na mgonjwa. Lakini kuna changamoto nyingi na mabadiliko mengi tunayopaswa kuyafanya katika kada hii kuanzia kwenye elimu, mazingira ya kazi, tabia na maadili na maono ya wauguzi na watu wengine juu ya uuguzi.
UUGUZI NA ELIMU
Uguuzi hapo kabla umechukuliwa kama kada ambayo isingehitaji ufaulu mkubwa kuweza kusoma, mabadiliko ya sayansi na teknolojia yamebadilisha hili kwenye jamii yetu lakini bado uuguzi huu unaotelewa kwa ngazi mbali mbali za elimu bado haujaonekana kama kada muhimu Zaidi kutokana na wauguzi wengi kuuchukulia uuguzi tofauti ya ile elimu wanayoipata mavyuoni. Wauguzi mbadilike hapa kwa kuitumia elimu tunayoipa mavyuoni kuleta mabadiliko kwenye kada hii . msifanye kazi kwa mazoea na badala yake tuongeze maarifa kwa kusoma na kujifunza zaidi ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa
Kusoma kutafanya tufanye kazi kwa weledi na kujiamini kwa huduma tutakayoitoa. Muuguzi anayejua vitu ni makini na ni tofauti na anaweza akagundua maendeleo mazuri na mabaya ya mgonjwa kwa kuwafatilia kwa ukaribu na kuepusha vifo visivyo vya lazima kwa wagonjwa.
MAZINGIRA YA KAZI
Mazingira ya kazi ya wauguzi wengi ni magumu na namba ya wauguzi bado haitoshelezi katika vituo vingi vya afya na hii itoshe kwa serikali kuongeza namba ya wauguzi Katika vituo vya afya ili kupunguza mzigo wa kazi. kumekua na upungufu mkubwa wa vifaa vya kazi katika vituo vingi vya afya. Serikali itie nguvu hapa katika kuongeza vifaa kwenye hospitali zetu na vituo vya afya.
Mazingira salama yenye vifaa bora na idadi ya kutosha ya wauguzi itaongeza hali katika kufanya kazi na kutoa huduma bora kwa wagonjwa na jamii kwa ujumla kwa sababu mazingira magumu na duni katika utoaji wa huduma ni miongoni mwa sabau zinazosababisha vifo vya wagonjwa katika hospitali zetu na vituo vya afya.
TABIA NA MAADILI
Wauguzi wanaonekana baadhi yao kukosa maadili mbele ya wagonjwa na kwa kazi yao kiujumla lakini hii haimaanishi kwa kila utovu wa nidhamu na ukosefu wa maadili kwenye vituo vya afya na mahospitali hufanywa na wauguzi lah si mara zote lakin hii ni kwa sababu ya picha iliyojengwa na wauguzi hapo kabla, ya kuwa ndio wanaokiuka maadili ya kazi zao.
Ili kufuta picha hii iliyotengenezwa miongoni mwa jamii zetu, wauguzi tubadilike hapa kwa kufata maadili ya kazi yetu tunapowaendea wagonjwa na jamii kiujumla. kuendelea kwa tabia mbaya na utovu wa nidhamu miongoni mwetu wauuguzi ni miongoni mwa vitu vinavyoirudisha nyuma kada hii.
Rushwa miongoni mwa wauguzi na tabia ya kupokea vitu kutoka kwa wagonjwa ili kutoa huduma ni miongoni mwa tabia tajika kwa baadhi ya wauuguzi. Ili tulete heshima katika kazi yetu ni muhimu kuachana na tabia zinazochafua kada ya uuguzi kama hii.
MAONO JUU YA UUGUZI
Maono juu ya uuguzi mengi yao ni hasi kuilekea kada hii muhimu kwenye sekta ya afya, na maono haya hasi huanza na wauguzi wenyewe, wauguzi wengi hujishusha na kujiona wa chini na kusahau uuguzi nao ni fani kama fani zingne na muuguzi hayupo pale kutumwa bali kusaidiaana na kada zingine kwenye utoaji wa huduma kwa wagonjwa na jamii.
Hali hii ya wauguzi kujiona wapo kazini kutumwa inawafanya wengi wao kushindwa kujiendeleza na kutotimiza majukumu yao ipasavyo. Tubadilishe maono yetu wauguzi juu ya uuguzi na kuleta mabadiliko chanya hii itasaidia kukuza kada hii na kuongeza namba ya wasomi kwenye uuguzi .TUJIINUE NASI TUTAINULIWA
Jamii nayo ina maono hasi juu ya uuguzi na hii ni kutokana na sifa na taswira iliyotengenezwa na baadhi wauuguzi juu ya kazi yao. Tutapobadilisha mtazamo wetu juu ya kada yetu na tutakapotimiza majukumu yetu na kufanya kazi zetu kwa bidii kwa kufata madili ya kazi hii itasidia kufuta taswira mbaya juu ya uuguzi iliyojengeka Katika jamii zetu .Tutakapo uangalia uuguzi kwa jicho na mawazo chanya itakua chachu katika kuboresha na kukuza kada hii muhimu katika sekta ya afya , mabadiliko katika mitaala ya elimu ya uuguzi na marudio yake yataboresha Zaidi fani hii muhimu.
WAUGUZI TUUNGANE
Wauguzi watakaposhikamana kuupeleka uuguzi mbele itasaidia Zaidi kuboresha utolewaji wa huduma za afya na hii ni kuanza kwa kubadilika nakufata yale yote ambayo uuguzi unahitaji . wauguzi tusijirudishe nyuma na kujiona duni tumekua kada ya muhimu kwenye afya kwa karne na karne na hii ni kutokana na umuhimu wetu kwenye swala zima la utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
Tuhimizane kwenye kusoma na kwenda na wakati kwa jinsi teknolojia inavyo kwenda juu ya mabadiliko yanayotokea katika kada ya uuguzi.
MUUGUZI MTU MUHIMU
Uboreshwaji wa mazingira ya kazi ya wauguzi,posho na mishahara ni vitu muhimu katika kuboresha kada hii ,na hii ni kutokana na kazi ,na umuhimu wa muuguzi. Muuguzi ndiye anaye kaa na mgonjwa muda mwingi ukilinganisha na kada zingine za afya muuguzi huyu huyu ndiye anaye fatiria na kujua maendeleo ya mgonjwa na mahitaji yake kwa ujumla.
Idadi ya waauguzi itakapo ongezeka makazini kwenye vituo vya afya na mahospitali itaongeza nguvu kazi katika utendaji kazi na utoaji wa huduma. Serikali ikaongeze kuajili idadi ya wauuguzi ili kuweza kuendana na uhitaji wa wagonjwa juu ya watoa huduma.
Muuguzi mtu muhimu tusimdharau
SHIME WAUGUZI SHIME

Upvote
5