The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Salaam Wakuu,
Nataka nizungumzie tu chembe ya uungwana ambayo inaweza kuwa na manufaa makubwa maishani mwetu.
Ni vema kuonesha uungwana unapopatiwa mkopo wa fedha na ndugu, jamaa au rafiki. Uungwana wa kwanza ni kuhakikisha una dhamira ya kulipa pindi unapokopa, kisha kupambana juu chini kuhakikisha unalipa.
Uungwana wa pili ingawa ni muhimu sana ni kuzingatia gharama (kama zipo) zilizotumika wakati wa kukopeshwa. Si vema kujisahaulisha kwenye hili.
Mfano: Wewe Taini umemuomba Juma kiasi cha Tsh 50,000 kisha akakutumia kwa njia ya benki au mtandao wa simu. Juma ametozwa Tsh 2,000 kukutumia hicho kiasi, halafu wewe Taini unamrudishia Juma Tsh 50,000 kamili bila kujali kuwa alitumia gharama fulani kukusaidia ulipokuwa na shida.
Amini, huenda aliyekutendea wema asikuulize jambo lolote ila huwa ni kipimo cha uungwana. Wakati mwingine anaweza kupata uzito kukusaidia kwakuwa huwa unabaki na buku buku zake mara kibao.
Haya makato ni sehemu ya mkopo. Usijisahaulishe. Unless mna makubaliano ya namna fulani kwamba kufanya hivyo hakuathiri mahusiano, uaminifu na zaidi, heshima iliyopo kati yenu.
Je, wewe ni muungwana wakati wa kurejesha deni? Je, umewahi kumshushia heshima mtu aliyekosa uungwana wa namna hiyo?