Uuzaji wa Mumiani (Maiti za watu wa kale)

Uuzaji wa Mumiani (Maiti za watu wa kale)

Zwangedaba

Member
Joined
Feb 1, 2009
Posts
99
Reaction score
25
Kipindi cha miaka 1800 wakati wa ushindi wa Napoleon huko Misri ulifungua historia ya Misri kwa Wazungu. Wakati huo, mumian hawakupewa heshima waliyostahili kutoka kwa wasomi wa Ulaya na kwa kweli, mumiani waliweza kununuliwa kutoka kwa wachuuzi wa mitaani - WAMACHINGA (kama inavyoonekana kwenye picha) an kutumiwa kama tukio kuu la hafla na mikusanyiko ya kijamii iliyofanyika katika karne ya 18. Wasomi wa zama hiyo mara nyingi walishikilia "Hafla za kuwavua mumiani", ambavyo, kama jina linavyoelezea, lilikuwa na mada kuu ambayo Mumiani angevuliwa mbele watazamaji wenye majivuno, wakshangilia na kupiga kelele kwa wakati mmoja.

mummy_trader_1865.jpg


Mmachinga akiuza mumiani mtaani (Misri 1865)

Katika kipindi hicho, mabaki yaliyohifadhiwa vizuri ya Wamisri wa kale yalikuwa yakisagwa kama unga na kutumiwa kama dawa. Kutokana na umaarufu wa jambo hili, ilipelekea kuwapo kwa udanganyifu katika biashara hii ili kukidhi mahitaji, ambapo miili ya waombaji ilitengenezwa kama ile ya Wamisri wa kale waliotumbuliwa na kutunzwa.

Kutokana na Mapinduzi ya Viwanda, mumiani wengi wa Wamisri walitumiwa kwa madhumuni zaidi ya kibinadamu: idadi kubwa ya mumiani wa binadamu na wanyama walisagwa na kutumwa Uingereza na Ujerumani kwa ajili ya matumizi kama mbolea. Wengine walitumiwa kama kikolezo (pigment) cha rangi ya kahawia au waliondolewa nguo zao, ambazo baadaye zilipelekwa Marekani kwa ajili ya matumizi ya kutengeneza karatasi viwandani. Mwandishi Mark Twain aliripoti kwamba mumiani walikuwa wakitumika pia kama nishati ya kuendeshea treni huko Misri.

Mwishoni mwa karne ya kumi na tisa, mumiani waligeuka kuwa vitu vyenye thamani kayika maonyesho, na mumiani walinunuliwa kwa wing na matajiri wa Ulaya na Amerika kama alama ya utalii. Kwa wale ambao hawakuweza kumudu mumiani mzima, mabaki yaliyogawanyika - kama vile kichwa, mikono au miguu - yaliweza kununuliwa kwa kificha (black market) na kusafirishwa nyumbani kisiri.

Kwa hiyo, tamaa ya biashara ya mumiani kwa Ulaya ilikuwa kubwa, kwamba hata baada ya kuyapitia, kuyafukua na kuiba kwenye makaburi yote hakukuwa na mumiani wamisri wa kale wa kutosha kukidhi mahitaji. Na hivyo mumiani bandia walitenegenezwa kutoka maiti za wahalifu waliouawa, wazee, maskini na wale ambao walikufa kutokana na magonjwa ya ajabu, kwa kuwazika katika mchanga au kuwajaza miili yao na lami na kuwakausha juani.

 
Tangu kale jamii mbalimbali walitumia mbinu tofauti kushughulika maiti. ...

Katika imani ya wengine ni muhimu kutunza maiti kwa namna fulani kwa sababu wanategemea kuwa mwili utarudishwa tena katika namna ya uhai. Imani hii ilikuwa msingi wa jitihada za watu wa Misri ya Kale waliokausha maiti kama mumia na kuyazika kiangalifu sana kwa sababu zilihitajika kwa maisha ya baadaye. (chanzo:https://sw.wikipedia.org/wiki/Maiti)
 
Mumia (kutoka ar. مومياء mumia, ing. mummy) ni maiti ya binadamu au mnyama iliyokauka bila kuoza. Hali hii inaweza kutokea kiasili katika mazingira maalumu au kwa kutumia mbinu fulani. Mchakato wa kuoza huzuiliwa na baridi kali, katika mazingira yabisi (pasipo na unyevu hewani) na mwendo wa hewa, kwa kukosa oksijeni au kwa kutumia kemikali fulani.

Jina la mumia lilitumiwa mwanzoni kwa kimiminika cha lami likawa jina kwa maiti yaliyokaushwa kwa kutumia lami yaliyopatikana hasa Misri likaendelea kutumiwa kwa maiti yote yaliyokauka bila kuoza.

Utamaduni wa Misri ya Kale unajulikana kwa dini yake iliyofundisha ni muhimu kutunza mwili ili mtu aweze kuzaliwa upya akiingia peponi baadaye. Wamisri walitumia mbinu mbalimbali kwa kutunza miili ya marehemu. Utumbo na ubongo vilitolewa na kutunzwa katika vyombo vya pekee baada ya kuvikausha katika chumvi. Mwili uliofunguliwa ulipakwa kwa chuumvi kwanza, baadaye na mchangnyiko wa nta, utomvu wa miti mwenye harufu nzuri na lami. Baadaye mwili ulizungukwa kwa bendeji za kitambaa kulicholoweshwa kwa madawa mbalimbali, pamoja na lami. Shughuli hizi zote zilitekelezwa na mafundi maalumu waliosimamiwa na makuhani. Wamisri ambao familia zao hawakuwa na uwezo wa kugharamia shughuli hizi zote waliandaliwa kwa mbinu sahili zaidi. Maskini walizikwa kwenye mchanga wa jangwa ambako mara nyingi maiti hizi zilikauka pia kabisa.

Wamisri walihifadhi pia miili ya wanyama hasa wanyama waliotazamiwa kuwa ishara ya miungu yao na kufugwa mahekaluni. Kwa jumla ni zaidi ya mumia milioni moja ya wanyama, hasa paka, zinazojulikana

Mumia asilia hutokea
  • kama mwili unatunzwa penye mchanga au mwamba unaonyonya kimiminika, hapa vimiminika kutoka maiti hupotea haraka hivyo bakteria zinazoozesha mwili hazina mazingira ya kustawi[7]
  • mumia zilipatikana mara kadhaa kama mtu walikufa katika migodi ya chumvi[8]
  • pale ambako mtu alikufa au alizikwa penye baridi, kwa mfano katika barafuto au kwenye taiga[9]
  • kama kuna upepo baridi mahali mwili unapokaa, kwa mfano ndani ya mapango kadhaa[10]
  • kama ardhi ya kaburi ina kemikali au asidi ndani yake zinazoua bakteria
Ilhali "mumia" ilikuwa kiasili miminika ya lami pekee neno hili lilitumiwa baadaye pia kwa maiti zilizokaushwa na kupatikana katika makaburi ya Misri ya Kale. Desturi ya kukausha na kutunza maiti kwa kutumia madawa mbalimbali ilikwisha baada ya mwisho wa dini ya Misri ya Kale kutokana na uenezaji wa Ukristo na baadaye Uislamu nchini. Lakini katika tabianchi yabisi ya Misri maiti za zamani zilikaa zikapatikana kwa wingi. Zilionekana nyeusinyeusi hivyo watu waliona zilitibiwa na "mumia" na kile cheusi kutoka makaburi kilitumiwa pia kama dawa. Baadaye matabibu wa Misri waliona kwamba ilifaa pia kutumia vipande vya maiti hizi kama dawa.. Baadaye wataalamu wa Ulaya, waliojifunza mengi kutoka tiba ya Waislamu, walipokea maelezo haya wakaanza kununua maiti zilizokaushwa kutoka Misri. Ilhali matumizi ya maiti kama dawa yalipungua katika nchi za Waislamu kuanzia karne ya 16 yaliendelea katika nchi za Ulaya hadi karne ya 19.

Soma zaidi hapa: https://sw.wikipedia.org/wiki/Mumia
 
Back
Top Bottom