Peter Agostino
Senior Member
- Sep 23, 2016
- 105
- 229
Mengi yamesemwa kuhusiana na hizi barakoa na hadi sasa hivi kuna baadhi ya watu hawajazielewa vizuri.
Kuna wanaodai zile za kutengenezwa mtaani hazifai kabisa lakini kuna kundi la watu wengine wanadai hata hivyo zinasaidia kuliko kuacha kabisa kuvaa.
Nilichokishuhudia leo kwa jirani yangu mmoja kwa kweli kimenisikitisha, Katoka na barakoa yake huko akatupita nje hata salamu akawa anatoa kwa shida alivyojifunga usoni na kuingia zake ndani.
Haukupita muda mrefu nikashangaa kumuona mwanawe mdogo wa miaka 4 akitoka na ile barakoa nje huku akiichezea. Si kama babake alijisahau hapana bali alimwambia mwenyewe, "Chukua mwanangu na wewe uchezee"
Vituko vingine ni pale utakapowaona watu wakijali zaidi uvaaji wa barakoa na kusahau njia zingine za kujikinga kama kunawa mikono na kukaa umbali wa mita moja.
Kwa mitindo kama hii ugojwa huu hatuwezi kuushinda, tujitahidi kuchanganya mbinu zote bila ya kudharau hata moja pale barakoa inaposaidia itumike lakini pale kukaa mbali kunaposaidia pia kutumike kikamilifu, kunawa mikono nk.