Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,036
- 9,331
MWAKA 1970, Umoja wa Mataifa (UN) ulipitisha azimio kuzitaka nchi zinazotoa misaada ya kimataifa kuongeza misaada hiyo ili ifikie asilimia 0.7 ya mapato ya nchi zao ifikapo 2015.
Moja ya nchi zilizotekeleza azimio hili ni Uingereza ambayo inasema imeongeza misaada yake hadi kufikia dola bilioni 18.93 mwaka 2013. Hii ni sawa na asilimia 0.72 ya pato lake la taifa. Nchi zingine zilizotimiza lengo la UN ni Denmark (0.84), Sweden (0.99), Luxembourg (1.0) na Uholanzi (0.71).
Ina maana kuna nchi nyingi zinazojiita wafadhili ambazo hazina hata matumaini ya kufikia lengo hili. Baadhi yao wamepunguza misaada wakati wakiongeza matumizi yao ya kivita.
Kwa kawaida ongezeko hili la misaada lingeshangiliwa, lakini asasi kadha za kiraia zimegundua kuwa
misaada hiyo iliyoongezeka ina malengo ya kuzisaidia kampuni zao badala ya wananchi walengwa. Kwa maneno mengine, mamilioni ya dola yanayotolewa kama misaada yanaendeleza miradi inayodhibitiwa na kampuni zao za biashara na kilimo.
Kwa njia hii kampuni za kimataifa kama Monsanto, Unilever na Nestlé zinazidi kupenya katika Bara la Afrika kwa kutumia mgongo wa misaada.
Ni kwa sababu misaada hii hutolewa chini ya mpango mpya unaoitwa mshikamano mpya kwa ajili ya usalama wa chakula na lishe (New Alliance for Food Security and Nutrition). Huu ni mpango ulioanzishwa huko Marekani mwaka 2012 na kikundi cha nchi nane tajiri (G8). Lengo lake ni kuendeleza uwekezaji kutoka nje katika nchi 10 za Afrika ambazo zimejiunga na mpango huu wa New Alliance.
Nchi zenyewe ni Ghana, Ethiopia, Tanzania, Cote DIvoire, Burkina Faso, Msumbiji, Nigeria, Benin, Senegal na Malawi. Wakati huo huo kampuni 50 za kimataifa kama Monsanto, Cargill na Unilever zimo katika mfumo huu. Chini ya makubaliano na G8 nchi hizi 10 zinatakiwa zitengeneze mazingira mazuri kwa ajili ya kuzikaribisha kampuni hizi.
Yaani chini ya mpango wa New Alliance wametuwekea masharti ili tupate hiyo misaada na mitaji mikubwa. Tunatakiwa tufanye mabadiliko katika sera zetu za ardhi, mbegu na biashara. Tunatakiwa turahisishe utaratibu wa kupata ardhi kwa wawekezaji wa kimataifa.
Tunatakiwa tuzuie utaratibu wa wakulima wetu kutumia mbegu zao wenyewe au za kienyeji. Ni lazima tueneze utumiaji wa mbolea za kemikali na sumu za kuua vijidudu katika mashamba yetu. Matokeo yake wakulima wanaingia gharama isiyo lazima na kuchafua mazingira pamoja na afya yao.
Baada ya kutengeneza mazingira haya ndipo wanatoa hiyo misaada na mitaji. Sehemu kubwa ya fedha hizi inasaidia uzalishaji mkubwa wa mazao kama tumbaku, pamba, mpira, michikichi na nafaka nishati.
Makubaliano haya chini ya New Alliance yanafanyika kisirisiri. Olivier de Schutter, mratibu wa masuala ya chakula katika UN, anasema serikali (za Afrika) zimekuwa zikitoa ahadi kwa wawekezaji nyuma ya pazia bila ya kufikiria mustakabali wa wakulima wadogo na bila ya kuwashirikisha.
Ndivyo, chini ya mpango huu wa New Alliance, Serikali yetu ya Tanzania imeahidi kuwa haitazuia usafirishaji wa chakula, hata kama chakula hicho kinahitajika na wananchi wetu. Kwa maneno mengine mpango huu unalenga kutosheleza mahitaji ya soko la kimataifa badala ya soko la ndani.
Ili kutekeleza mpango huu wameanzisha miradi wanayoita kanda za maendeleo ya kilimo (Agricultural Growth Corridors) inayosimamiwa na kampuni za kimataifa. Lengo wanasema ni kutusaidia kuendeleza ardhi yetu kwa kuongeza mazao, kwa sababu wanasema ardhi yetu haitumiki vilivyo. Pia wana mipango ya kuunda miundombinu ili kurahisisha mazao ya kilimo kusafirishwa hadi bandarini kwa ajili ya kutoa nje.
Tayari wameanzisha kanda mbili nazo ziko Msumbiji (Beira Agricultural Corridor au BAGC) na Tanzania (Southern Agricultural Corridor of Tanzania au SAGCOT).
Ni dhahiri kuwa mpango huu wa New Alliance hauna lengo la kutosheleza mahitaji ya chakula na lishe ndani ya nchi zetu, bali nia ni kuzifanya kampuni za kimataifa ziwe zinadhibiti ardhi yetu na mazao yake kwa ajili ya soko la kimataifa.
Ndio maana msemaji wa BAGC alimwambia mwandishi wa gazeti la Guardian (Uingereza) kuwa: Tunakusudia kuweka uzito zaidi katika uzalishaji wa mazao ya biashara. Tunataka mkulima mdogo aingi(zw)e katika biashara hii. Hatuhusiki na maslahi ya kijamii
Bila shaka kwa kusema hawahusiki na maslahi ya kijamii alimaanisha uzalishaji wa chakula kwa ajili ya kuilisha jamii. Kulima kwa ajili ya soko la nje maana yake ni kutegemea chakula kutoka nje, kinachonunuliwa kwa bei inayopangwa nje. Mwaka 2008 uchumi wa dunia ulipodorora bei ya chakula ilipanda nasi tukalazimika kununua kwa bei ya juu. Haya ni matokeo ya kutegemea chakula kutoka nje.
Mpango huu pia una sura nyingine. Nayo ni njia ya kampuni za kimataifa kujipatia ardhi. Wanachodai ni kuwa katika maeneo ya kanda kuna ardhi nyingi ambayo haitumiki na kwa hiyo ni vizuri kuitumia ili iweze kuleta tija. Ukweli ni kuwa sehemu kubwa ya ardhi wanayochukua inakaliwa na wananchi ambao wanailima. Kwa hivyo matokeo yake ni wakulima wadogo wengi wanapokonywa ardhi inayowapatia riziki ili wawekezaji waitumie.
Ndio maana chini ya mpango huu wa Alliance nchi za Kiafrika zinatakiwa zibadilishe kanuni na sheria zao kuhusu umiliki wa ardhi na mambo mengine kadhaa. Tayari hatua 200 zimechukuliwa na nchi wanachama.
Kwa mfano Ethiopia imeweka utaratibu wa wawekezaji kupewa ardhi fasta fasta yaani bila ya urasimu. Tayari katika nchi hiyo wawekezaji wamekwishakuchukua hekta milioni 63 tangu mwaka 2008. Tena wamepewa ofa za muda mrefu.
Na nchini Malawi serikali imeahidi kutenga hekta 200,000 zenye rutuba kwa ajili ya wawekezaji wakubwa ifikapo 2015. Huko Ghana nako zitatolewa hekta 10,000 ifikapo mwisho wa mwaka ujao. Nigeria imeahidi kuwa itabinafsisha kampuni za umeme. Hivi ndivyo tunavyotekeleza huu mpango mpya wa kuendeleza kilimo.
Halafu kampuni hizi siyo tu zinadhibiti mazao yanayotokana na ardhi zetu bali pia zinadhibiti pembejeo zinazotumika katika kilimo, yaani wanadhibiti kinochotoka na kinachoingia ardhini. Kwa mfano kampuni za Monsanto, Syngenta na DuPont zinalenga kuongeza biashara yao ya mbegu katika Afrika.
Lengo ni kudhibiti uzalishaji na usambazaji wa mbegu, hivyo mkulima atapoteza haki ya kutumia mbegu zake anazoweka akiba kama ilivyo kawaida ya miaka yote. Tayari Msumbiji imeahidi kuzuia usambazaji wa mbegu za kienyeji.
Hivyo, mkulima mdogo anayeilisha Afrika kwa hivi sasa atajikuta anapoteza uwezo wake akiwa anatawaliwa na kampuni za kimataifa. Huu ni uvamizi wa pili wa Afrika, sawa na ule wa mwaka 1884-85 wakati wakoloni walipokutana huko Berlin na kujigawia maeneo ya Afrika. Ule ulikuwa ukoloni mkongwe na huu sasa ni ukoloni mamboleo.
Makundi takriban 100 ya wakulima katika Afrika yametangaza kuwa mpango huu wa Alliance ni ukoloni mambo leo unaojiingiza katika bara hili. Wanasema hizi ni njama za nchi tajiri na kampuni zake kudhibiti ardhi na maliasili zetu.
Makundi haya yanaungwa mkono na asasi ya kimataifa inayoshughulika na maendeleo (World Development Movement au WDM) ambayo imewashauri wafadhili waachane na mradi huu wa Alliance. Badala yake misaada yao itumike kuwasaidia wakulima wadogo, ili waweze kudhibiti ardhi yao, jasho lao na mazao yao. Yaani misaada inayotolewa iweke mbele mahitaji ya chakula ndani ya nchi badala ya kutumikia maslahi ya wawekezaji kutoka nje.
WDM imeitaka Uingereza iache kutumia dola bilioni moja katika mpango wa Alliance. Badala yake fedha hizo zitumike kuwezesha sera na miradi inayoendeleza uhuru wa chakula kwa wananchi. Hii inaweza kufanyika kwa kuwasaidia wakulima wa Afrika kudhibiti ardhi na maliasili zao kwa madhumuni ya kuzalisha chakula kwa ajili ya soko endelevu la ndani.
Naye Kato Lambrechts, ofisa mwandamizi wa asasi ya kimataifa Christian Aid anasema: Serikali za Kiafrika zimesaini mikataba kuunda sera na kutunga sheria ambazo ni vizuri zingejadiliwa kwa kina na wananchi ndani ya nchi zao. Ni kwa sababu wanasukumwa kuchukua hatua hizi ili kuwavutia wawekezaji wakubwa katika sekta ya kilimo
Anaongeza kuwa kinachohitajika ni sera za kimaendeleo zitakazolinda maslahi ya mkulima masikini ili atokane na hali hiyo.
--- Imenukuliwa ilivyo kutoka kwenye gazeti la RAIA MWEMA, imeandikwa na Nizar Visram