Lady Mwali
Senior Member
- Nov 15, 2018
- 147
- 333
Kutokana na hasara kubwa waliopata wafanyabiashara wa soko la Karume baada ya ajali ya moto ni busara na ubinadamu wa hali ya juu Umoja wa Vijana wa CCM ufanya harambee ya kuchangisha pesa kwa ajili ya kuwapunguzia machungu wahanga hawa wa moto.
Najua UVCCM wanna ushawishi mkubwa kwa viongozi na matajiri wa nchi hii, hilo linawezekana madiwani, wabunge, wakuu wa mikoa na viongozi wengine waoneshe utu wa kuchangia wahanga hawa wa ajali ya moto.
Hata mama Samia aoneshe utu wake kwa kuchangia pesa akionesha njia kwa viongozi wengine hakuna ubishi wafanyabiashara wa soko hili wamepoteza mitaji yao yote ukizingatia walio wengi wana mikopo benki, wataishi vipi na familia zao?
Napenda kampeni hii ianze mara moja hii itaonesha jinsi gani CCM inajali wananchi na ni kipimo tosha cha kuonesha utu na ubinadamu.