Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Geita umeeleza dhamira yake ya kuendelea kuwalinda na kuwaunga mkono viongozi wanaojitolea kujenga na kuimarisha chama, ikiwemo kusaidia ujenzi wa ofisi za chama katika maeneo mbalimbali.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita, Manjale Magambo, alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake katika kata 17 za Wilaya ya Mbogwe. Alisema vijana wa UVCCM wanaridhishwa na juhudi za viongozi wanaochangia maendeleo ya chama kwa kuboresha ofisi za kata na mashina, hatua ambayo inaendelea kukipa heshima Chama Cha Mapinduzi.