Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi UVCCM Mkoa wa Geita imewataka baadhi ya Wabunge pamoja na Madiwani wanaojipitisha katika Maeneo mbalimbali na kuhalalisha mitano tena kupitia nafasi zao kuacha mara moja kwani ni kosa kwa mujibu wa taratibu za Chama.
Hayo ameyaeleza Mwenyekiti wa Umoja huo Manjale Magambo wakati alipofanya ziara ya kutembelewa wanachama wa jumuiya hiyo wilayani Nyangh”wale kwa lengo la kuhamasisha vijana kujitokeza kuchukua fomu za uongozi , kuona uhai wa chama hicho pamoja na kuchangamkia fursa za Mikopo ya asilimia 10.