UVCCM hili jukumu mmepewa na serikali au hamna kazi ya kufanya?

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
DIRISHA LIMEFUNGULIWA, NJOO TUKUSAIDIE KUFANYA APPLICATION ZA MKOPO BODI YA MIKOPO HESLB.

Contacts:- 0627799285. Katibu Seneti Mkoa

Habari!
Dirisha la Kufanya Maombi ya Mikopo Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) limefunguliwa.

Uongozi wa UVCCM kupitia Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Seneti (M) Kilimanjaro kwa kutambua kuwa Waombaji wengi wamekuwa wakipata Changamoto ya Kufanya Maombi kwa Usahihi, tumejiandaa Kuwasaidia Wanafunzi wote wanaotarajia kufanya Application HESLB bila Kujali itikadi za Kisiasa, na Usaidizi huo utafanyika Bure bila Malipo.

Hivyo kwa Mwanafunzi au Mwananchi yeyote anayehitaji kufanya LOAN APPLICATION HESLB karibu Ofisi za UVCCM (M) Kilimanjaro na Utapata Usaidizi na kufanyiwa Application bila Malipo.

Ni kila siku za Kazi kuanzia Saa tano asubuhi Mpaka Saa tisa Jioni.

Kwa Mawasiliano au Maulizo Wasiliana na Katibu Seneti Mkoa No. 0627799285
Goodluck N. Bosha.

KARIBU TUJENGE TAIFA IMARA PAMOJA. WEWE NDIO FUTURE.
 
UVCCM kuwa na matawi ndani ya taasisi za elimu ni hatari inazalisha mbumbu vyuoni.

Badala ya kusoma ili upate maarifa,a ujuzi, unasoma ili kupata connection na akili huna.
 
Bavicha nao wakaja na mabango , hiyo mikopo itatosha!!

Mikopo mnakopeshana,kuzalisha wasomi wa kwenda kuendesha boda boda na mikopo yenyewe hailipiki.
 

Attachments

  • IMG-20240609-WA0005.jpg
    121.8 KB · Views: 3
Kumekuwa na kipindi wanafunzi wanapoomba mikopo ya elimu ya juu, mara nyingi wanaenda ofisi ya umoja wa vijana wana apply. Ninachojiuliza UVCCM ni mawakala wa bodi ya mikopo? wengi wao wamesema imekuwa rahisi kupata mikopo kupitia ofisi za umoja huo. Kwa style hiyo vijana wengine wanaweza kukosa fursa kwaajili ya mambo ya kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…