Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Comrade Faris Buruhani, ameungana na Waislamu wa wilaya ya Missenyi na Mkoa wa Kagera kwa ujumla katika Maulid ya Bwana Mtume Mohammad [s.a.w] iliyosomwa katika Kata ya Kyaka wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.
Akitoa salamu za Chama na Jumuiya mbele ya maelfu ya waumini hao, amewasihi viongozi wote wa dini mkoani Kagera kuwahimiza na kuwakumbusha waumini wao kushiriki ipasavyo katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, kwa kuchagua viongozi wazuri watakaokuwa chachu ya maendeleo katika mitaa na vijiji vyao.