UVCCM: Katiba mpya iwe na ibara ya kuwa na wake zaidi ya mmoja.....

UVCCM: Katiba mpya iwe na ibara ya kuwa na wake zaidi ya mmoja.....

only83

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
5,343
Reaction score
2,527
Wakati nchi ikiwa kwenye mchakato wa kupata katiba mpya itakayokaa badala ya ile ya 1977, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM), wemetoa maoni yao kuwa ni vyema katiba mpya ikawa na ibara inayoruhusu mke zaidi ya mmoja. Wakichangia kwenye baraza lao mkoani Morogoro, vijana hao walidhihirisha tabia yao kwa kuongea wakiwa serious kabisa kuwa wanataka kuoa wake wengi iwe ni ibara ndani ya katiba.

ITV news bulletin saa tano.

My Take:

Haya ndio maoni ya vijana wa CCM, kwa Muungano sio hoja, maliasili sio ishu, nk, wao wanawake kwanza.
 
Sijaangalia ITV,lakini nashindwa kuamini kama kweli hawa wenzetu wamefilisika kiasi hiki.Yaani matatizo lukuki wewe unajadili kuongeza mke?Sisi tunataka kurudisha hata huyu mmoja aliyepo wao wanaomba kuongeza?Kwani katiba ya zamani inakataza kuoa wake zaidi ya mmoja?
 
kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake......nami nasema iwepo ibara ya kupinga mahusiano na ndoa za jinsia moja
 
Kama hivyo ndivyo basi katiba itambue wanawake kuolewa na mwanaume zaidi ya mmoja mia.
 
hakika ccm ni majanga,ni vijana wasiojitambua tu wenye mawazo muflis kama hayo.
 
Kama hivyo ndivyo basi katiba itambue wanawake kuolewa na mwanaume zaidi ya mmoja mia.

kama utatoa maoni hayo hautazuiwa,kila mtu na maoni yake. hata ukitaka haki ya kupiga punyeto kwenye katiba ni wewe tu.
 
Back
Top Bottom