Pre GE2025 UVCCM Mkoa wa Kagera Yazindua na Kukabidhi Nyumba ya Mama Asimwe

Pre GE2025 UVCCM Mkoa wa Kagera Yazindua na Kukabidhi Nyumba ya Mama Asimwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WhatsApp Image 2024-12-07 at 20.30.18.jpeg

📍Izigo_Muleba
🗓️Tarehe 07/12/2024

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Comrade Faris Buruhani, ameongoza uzinduzi na makabidhiano ya nyumba ya Mama Asimwe sambamba na chumba kimoja cha biashara. Tukio hilo limefanyika leo tarehe 07/12/2024 katika kata ya Izigo, wilaya ya Muleba.

WhatsApp Image 2024-12-07 at 20.30.19 (1).jpeg

Makabidhiano hayo yamekuja baada ya ukamilishaji wa ahadi ya Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Kagera kwa Mama Asimwe, ya kumboreshea mazingira yake ya kuishi kwa kumjengea nyumba ya kuishi na chumba kimoja cha biashara.

WhatsApp Image 2024-12-07 at 20.30.20.jpeg

Ni miezi 6 sasa imepita tangu tukio la ajabu na la kikatili la Mauaji ya Mtoto asiye na hatia Asimwe Novat, aliyekuwa na ulemavu wa ngozi (Albino) litokee na kuacha simanzi kubwa kwa mwana dada Judith Richard (Mama Asimwe) na jamii nzima ya watanzania.

WhatsApp Image 2024-12-07 at 20.30.20 (1).jpeg

ASANTE MUNGU WETU KWA KUTUFANIKISHIA HILI
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-12-07 at 20.30.19.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-07 at 20.30.19.jpeg
    352.9 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-12-07 at 20.30.19 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-07 at 20.30.19 (2).jpeg
    472.2 KB · Views: 4
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, umemkabidhi nyumba yenye thamani ya Sh12 milioni mama mzazi wa marehemu Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, aliyeuawa kikatili na kunyofolewa viungo na watu wasiojulikana.

Mtoto Asimwe Novath (2) alitekwa Mei 30, 2024, usiku, akiwa mikononi mwa mama yake katika kijiji cha Bulamula, wilayani Muleba. Juni 14, 2024, baadhi ya viungo vya mwili wake vilikutwa vimetupwa ndani ya mfuko wa sandarusi chini ya daraja barabara ya Ruhanga Makongora, kata ya Ruhanga.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa nyumba hiyo, leo Jumamosi, Desemba 7, 2024, mama huyo, Judith Richard, amesema nyumba hiyo ni faraja kubwa kwake.

"Namshukuru Mwenyekiti wa UVCCM Kagera na wote waliowezesha hili. Machozi yangu yamefutwa, na sasa ni wakati wa kupambania maisha yangu na ndoto zangu," amesema Judith.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM Kagera, Faris Buruhan, alisema wamekabidhi nyumba hiyo yenye vyumba viwili, fremu ya biashara, kiwanja cha robo eka na mashine ya kushona nguo.

"Hii ni ahadi tuliyoitoa baada ya tukio lile la kusikitisha. Tunashukuru wadau waliotuwezesha kufanikisha ujenzi huu," amesema Faris, akiahidi kuendelea kumsaidia mama huyo.
 
Back
Top Bottom