Ktk chuo kikuu cha dodoma kunaendelea kampeni za kumchagua raisi wa chuo ila imeonekana wazi serikali kupitia uongozi wa juu wa chuo kuwaweka watu wao wanawowataka wao kwani Abubakary Bashe nduguye wa Bashe aliyeambiwa siyo raia wa TZ akiwa ktk kampeni zake za Udom akikana yeye siye ccm na hayupo ktk UVCCM ila alijikuta akitumia mda mwingi akizidumisha fikra za mwenyekiti JK alizokuwa akizungumza ktk kampeni na mpaka sasa ktk madaraka yake mambo hayo ni;
1. Ukabila
2. Dini
3. Ukanda
4. Uwanaharakati ( chadema)
Wana JF chukua maneno ambayo mwenyekiti wa ccm huwa akizungumza ktk hayo mambo manne kisha paste kwa uyo Abubakary Bashe ndivyo alivyokuwa akisema.
My take:
Udom ni sehemu ya wasomi badala ya kuzungumzia academic issue yeye anatoka nje ya mada na inaonesha wazi kuacha mambo ya masomo na kawekwa kwa sababu maalumu.
Kwani Udom inamatatizo mengi sana ya kitaaluma.
Wana Jf wenzangu wana UDOM wamekuwa wakipotosha taarifa nyingi juu ya uchaguzi huu wa URAIS,hoja na mantiki zinazotumiwa kumchafua huyu dogo anaetwa ABUBAKAR MOHAMED,ni kwakuwa tu ni mdogo w HUSSEIN BASHE, dogo huyu kiukweli ni kichwa ameweza kujipambanua kwamba yeye si mamluki wa CCM collage ya education si kweli alifukuzwa haya anayoyasema yalitokana na maswali tuliomuuliza mwenyewe,mfano aliulizwa uhusino na kaka yake,alijibu akasema ni kweli Hussein ni kaka yake,lakini akashangaa watu kumuhukumu undugu wa kaka yake wasidhani na yeye ni ccm,alihoji 1995 makongoro nyerere alikuwa NCCR, leo mjukuu wa mwalimu nyerere ni chadema haina maana ukitoka ktk familia ya wana ccm basi na wewe ni ccm dogo alisema huo ni uvivu wa kufikiri,aliwakumbusha wana udom kwamba asihukumiwe kwa jina la kaka yake bali matendo yake.
iliibuka hoja ya udini akaambiwa inakuaje collage ya education wagombea wote waislamu,akajibu ni mvivu wa fikra tu ambae atahoji hilo na kusahau kwamba viongozi wa collage hiyo miaka yote hawajawahi kuwa waislamu na hoja hii haijawahi kuibuka kwanini sasa?akawashangaa waalimu wenzangu hapa udom ambao tunaleta hoja ya dini,akasema ukiona watu wanajadili DINI,KABILA,UKANDA dogo alitumia maneno yafuatayo,either ni wendawazimu,ama ni wavivu kufikiri ama wana maradhi ya kumbukumbu.alishangaa wasomi kuanza kufikiri katika muelekeo huo,na alituonya tusiwe tunafikiri kwa urefu wa pua zetu KAMA VIONGOZI WENGI WA NCHI HII .
Dogo huyu alisema yeye si mwana ccm kwakua ccm ya sasa si ile aliyoienzi mwalimu nyerere,alisema yeye si cuf kwakua chama hichi si cha kitaifa,alisema yeye si nccr,kwakua chama hichi si cha upinzani,alisema yeye si chadema kwakuwa mpaka sasa chadema kimekaa kiharakati na kushindwa kujenga chama na kimeanza migogoro ya kimakundi kama ccm,ila alimalizia kwa kusema mpaka sasa hana kadi ya chama chochote ila anakitazama kwa ukaribu chama cha chadema kwani anahisi kinaweza kujibu matatizo ya watanzania kikiamua kufanya kazi ya chama cha kisiasa kwani hata 201o,alipiga kura kwa DK SLAA,UBUNGE HAKUCHAGUA ,UDIWANI ALICHAGUA CUF,na alisema aliharibu kura ya ubunge kwakua mgombea wa chadema wilayani kwake hakua na sifa,na kamwe asingechagua CCM.
Wana JF si kweli tulimfukuza bali huyu ni mgombea pekee ambae aliweza kufanya kampeni ktk collage yetu CCM hawana imani nae kwakuwa wana hisi si mwenzao huyu ni mgombea pekee ambae ametuahidi mabadiliko ya katiba,ni mgombea pekee aliejibu swali linalohusu infomartics namna atakavolitatua,ni mgombea pekee alietuahidi kumfikisha polisi RAIS wetu anaemaliza muda wake kwa UFISADI alofanya ni mgombea pekee alietuahidi kutoruhusu ccm kukitumia chuo chetu kwa maslahi yao,ni mgombea pekee alietuahidi kusimami swala la mafunzo ya vitendo.
Ni aibu watu kuja hapa na kupotosha haya mengi