Pre GE2025 UVCCM - Temeke yawakumbuka wenye uhitaji kuadhimisha miaka 48 ya CCM

Pre GE2025 UVCCM - Temeke yawakumbuka wenye uhitaji kuadhimisha miaka 48 ya CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Umoja wa vijana chama cha mapinduzi wilaya ya Temeke umesema utaendelea kuishi kwa vitendo malengo ya kuasisiwa kwa Chama Chama Mapinduzi CCM kwa kuwajali watu wote kwani Chama hicho ndio kimbilio la wanyonge

Wakizungumza wakati wa Matembezi maalumu yaliyokwenda sambamba na kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Kurasini ikiwa ni mwendelezo wa Shamrashamra za miaka 48 ya kuzaliwa kwa chama hicho Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Temeke na Mkimbia mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024 Maria Mapunda amesema dhamira ya CCM ni kufikisha huduma muhimu kwa wananchi kwani watu wote ni sawa na Afrika ni moja

Huku Katibu wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Temeke Sai Samba amesema pamoja ma mambo mengine matembezi hayo yamelenga kuunga mkono Azimia la Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Taifa uliofanyika Dodoma pamoja na kuwapongeza wagombea Urais mwaka 2025 kwa tiketi ya CCM ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Mgombe mwenza ambaye ni Balozi Dkt Emmanuel nchimbi na Dkt Hussen Mwinyi kwa upande wa Zanzibar.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Back
Top Bottom