Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
UVCCM KWENYE VITA YA MAFUTA TUPO UPANDE GANI?
Na Elius Ndabila
0768239284
Mjadala mkubwa kwa Taifa letu ambao unashika kasi kila kuitwapo leo ni kupanda Kwa gharama ya maisha kuliko sababishwa na ongezeko la mafuta mara dufu.
Mjadala huu umepamba moto Kwa miezi miwili na ushea sasa. Lakini chombo kikubwa ambacho ndicho jicho la Chama au Askari Mwavuri wa Chama katika kuisimamia serikali na kuwasemea vijana wapo kimya. Sijasikia idara hii muhimu ndani ya Chama ikiitetea serikali au ikiwasaidia Wananchi kupaza sauti juu ya kero hii ya kupanda Kwa gharama za maisha kunakotoka na kupanda kwa bei ya mafuta.
Vijana ndio think tank ya Taifa ambao inaaminika wanaweza kufanya tafiti na kuja na majawabu ya kukisaidia Chama na Serikali yake. Mimi ninajiuliza, UVCCM inamsubiria Katibu Mkuu Chongolo au Katibu Mwenezi Shaka aseme ili waje kupongeza? Kazi ya jumuiya siyo kuandaa makongamano ya kupongeza na jogging TU, malengo makubwa ya Vijana ni Askari wa Chama. Hawa ndio jicho la chama katika maisha ya kila siku. Hawa ndio wanapaswa kuwa wa kwanza kukemea au kupongeza bila kujali kukosea. Mhimu wao ni kutumika kama amplifier ya Chama kabla Chama hakijasema.
Ukimya huu wa Jumuiya yetu wakati watu wakiteseka inaonyesha hatuna mawazo kinzani juu ya hiki kinachoendelea. Rais wetu ana kazi nyingi, hawezi kusema kila kitu. Katibu mkuu wa CCM ana majukumu makubwa, nyie UVCCM ndio jicho lake.
Leo kuna kundi limeibuka Kwa kudai kodi za mafuta ni kubwa mno ndiyo maana mafuta yapo juu. UVCCM tunashindwa kuwajibu kuwa kodi hizi zipo kwa muda mrefu na si kipindi hiki Cha Mhe Samia tu? Hatuoni wanaolalamikia kodi kuwa kubwa wanajaribu kumtwisha Rais mzigo kuwa ndiye ameziweka wakati Toka zamani zilikuwepo? Wabunge hizi kodi hawakuzijua ndo wanazijua Leo? UVCCM changamkeni, acheni kujitenga na matatizo. Si kazi ya Chama kujibu kila kitu, ila ni kazi ya jumuia ku-react kwenye kila kitu.
Mimi nimetumia haki yangu kuwakumbusha wajibu wenu na kuwaondoa kwenye usingizi mzito. Hakuna Wilaya iliyotoa tamko Wala mkoa na Taifa. Na nyie mumekuwa sehemu ya Watazamaji wakati serikali ni yetu. Tunataka BAVICHA ndio waje kuwasaidia Wananchi kupiga kelele?
Mwisho ninalishukuru Bunge Kwa kusikia kelele za Wananchi na kuanza kupaza sauti. Huo ndio utumishi na uwakilishi wa Wananchi. Punguzeni Kodi Ili ku rescue gharama hizi. Maisha huku mtaani ni magumu. Na huko mbele yatakuwa magumu zaidi Kwa kuwa wakulima wengi walishindwa kulima kutokana na pembejeo za kilimo kuwa unaffordable.