Katibu wa umoja wa vijana wa CCM Khenan Kihongosi amemuonya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza bwana Diallo kuwa aache upotoshaji mara moja, kitendo cha kusema baadhi ya viongozi waliopita walitakiwa kuwa Mirembe ni cha kipotoshaji kwani Diallo yupo kwenye vikao vyote vya maamuzi kwani ni mjumbe wa kamati kuu.
===
CCM imelaani kauli ya kubeza viongozi wastaafu iliyotolewa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mwanza, Antony Diallo katika mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha televisheni nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Julai 10, 2021 na katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM), Kenani Kihongosi katika kikao cha majumuisho ya ziara ya kuimarisha chama inayofanywa na sekretarieti ya chama hicho ikiongozwa na katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.
Kihongosi amesema kauli iliyotolewa na kiongozi huyo ni msimamo wake mwenyewe na si wa CCM na kwamba jumuiya ya vijana inalaani kauli zinazotolewa na kiongozi huyo kuwabeza viongozi walioitumikia nchi, akitaka wastaafu hao kuachwa wapumzike.
"Tangu leo asubuhi tumeona ujumbe ukisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kauli iliyotolewa na mmoja na kiongozi ambaye anaingia kwenye vikao vya maamuzi lakini leo ameamua kutoa kauli hii ambayo imetuchukiza sana vijana kwani tulitegemea wawe wa kwanza kutuongoza, " amesema.
Kihongozi amesema kiongozi huyo wa CCM ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amenukuliwa akisema viongozi wengine wanaoteuliwa na CCM wanapaswa kuwa hospitali ya magonjwa ya akili ya Mirembe iliyopo mkoani Dodoma.

Sita washangaa,ila itakuwa ni bahati kwake kama ikawa ni hatua hiyo tu,ila inasemwa kuwa tenda wema usisubiri shukrani yeye,katekeleza wajibu wake kuwakumbusha kuwa walisha toka nje ya misingi ya taifa hili,wao wananuna.
Timu magufuli mareheme mmeshikwa kunako na mwana ccm mkongwe zaid ya marehemu na ninyi mikia yake. Kama alikuwa hafai ni hafai tu wala sio siri hatuwezi kuitukuza maiti iliyo litesa taifa kwa miaka mitano
UVCCM waongea kwa uchungu mkubwa kufuatia kauli ya Mwenyekiti wa CCM wa mkoa
UVCCM watoa kauli ya kulaani vikali kauli hiyo ya Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza.
UVCCM yamuomba Katibu Mkuu wa CCM kuongea na Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Mwanza Dr. Anthony Diallo.
. Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndugu Kenani Laban Kihongosi amesema umoja huo unaikemea na kuilaani vikali kauli Iliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii akisema kuwa kipindi cha nyuma kuna viongozi walichaguliwa kuongoza wakati wana rekodi ya kuwa vichaa na walitakiwa kuwa 'Milembe' badala yake wakapewa kuongoza nchi.
Ndugu Kihongosi amesema kuwa UVCCM imesikitishwa na kauli hiyo ya uongo ambayo pia si ya kiungwana inayolenga kutweza na kudhalilisha viongozi waliowahi kuongoza nchi sambamba na kukosa maadili ya uongozi kwa mujibu wa taratibu za chama.
"Tumesikia maneno ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza tunaamini chama chetu, kiko makini katika kusimamia maadili ya viongozi wake, UVCCM tunaamini Chama kitatafakari na kuona namna nzuri ya kushuhulikia jambo hilo kwa mujibu wa kanuni za uongozi na maadili." Alisema Kenani Kihongosi
Amefahamisha UVCCM inaamini kuwa viongozi wa chama wanatakiwa waongozwe na busara na hekima pindi wanapozungumza kuliko kuongea mambo ambayo yanaleta ukakasi na kudhalilisha Chama na Serikali jambo ambalo linakwenda kinyume na maelekezo ya kanuni za maadili na uongozi.
"UVCCM tunaikemea na kuilaani vikali kauli hiyo, Viongozi wetu waliopita waachwe wapumzike na waheshimiwe baada ya kutekeleza majukumu yao, yeye kama aliona hivyo alibakia kwenye chama kufanya nini? Akitokea kiongozi wa namna hii anakiuka maadili ya chama chetu sisi UVCCM tutanyoosha mstari kulinda kanuni na maadili ya chama chetu," Alisisitiza Kihongosi.
Halafu najiuliza hawa UVCCM walikuwa wapi wakati kina hapi, musiba , na wengineo wana wasema vibaya wastaafu eti leo mungu wao kuambiwa ukweli wa tabia zake wana ibuka na vioja.
soma katikakati ya mistari...ni daktari anayeweza kuthibitisha fulani ni kichaa... kupitia report ya daktari ndio tunaweza kuthibitisha hilo....umeshawahi kuiona hiyo report ya daktari?.....