Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
UVCCM YAGAWA SIMU 20,KADI ZA CCM 8,000 NA UVCCM 1,000 KUZIDI KUIMARISHA USAJILI WA WANACHAMA KIELEKTRONIK, MKOA WA LINDI
Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa Vijana wa CCM ndugu Mohammed Ali Kawaida jana tarehe 12 Septemba,2024 amewasili Mkoani Lindi kwaajili ya Hamasa day katika wilaya ya Luangwa.
Mwenyekiti Mkoani Lindi amesaini vitabu pamoja na kupokea taarifa ya Chama pamoja na Jumuiya zake lakini pia kugawa simu 20, kadi za CCM 8000, kadi za UVCCM 1000 lengo likiwa ni kuimarisha Chama na Jumuiya pamoja na kuongeza kasi ya Usajili wa wanachama wa CCM na UVCCM kielektroniki.
Lengo la hamasa day kwanza ni kuhamasisha vijana kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kujiandikisha, kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali kwa wenye sifa pamoja na kujitokeza kupiga kura siku ya uchaguzi,
Malengo mengine ya Hamasa day ni kuwaeleza wananchi ni kwa namna gani serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na CCM inatekeleza Ilani ya Uchaguzi wa 2020 - 2025
#KijanaNaKijani
#TunazimazoteTunawashaKijani
#UVCCMKazini
Imetolewa na Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-09-13 at 15.47.38.jpeg114.6 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-09-13 at 15.47.21.jpeg82.6 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2024-09-13 at 15.47.27.jpeg87.5 KB · Views: 0 -
WhatsApp Image 2024-09-13 at 15.47.22.jpeg103.7 KB · Views: 0 -
WhatsApp Image 2024-09-13 at 15.47.23.jpeg109.9 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2024-09-13 at 15.47.25.jpeg117.4 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2024-09-13 at 15.47.29.jpeg118.3 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2024-09-13 at 15.47.32.jpeg120.2 KB · Views: 2