SoC01 UVIKO -19 inavyodhibitiwa

SoC01 UVIKO -19 inavyodhibitiwa

Stories of Change - 2021 Competition

ADAM SADAM

New Member
Joined
Sep 16, 2021
Posts
3
Reaction score
3
Ndugu wazalendo wana JamiiForums hususani jukwaa la Stories of Change Kwa afya niliyonayo leo ninawaombea wote pia Mungu awaunganishe na Mimi katika andiko langu hili mkiwa na afya njema mungu awabariki na awaepushe na tatizo lolote la kiafya, Leo nitachambua kinagaubaga juu ya ugonjwa hatari kabisa ulioikumba dunia ukijulikana kama UVICO -19

NINI MAANA YA UVICO -19
Imekuwa ikiwachanganya sana watu maana UVICO-19 NA COVID- 19 Kuanzia Leo usibabaishwe tena na maneno haya yote yana maana ile ile, wizara ya afya ilitafsri kwa lugha yetu ya kiswahili ikiwa ni kifupi cha maneno Ugonjwa (U)wa Virusi(VI)vya Covidi(CO)alafu 19 ni mwaka ambapo kwa Mara ya kwanza viligundulika huko China 2019 vilevile kirefu cha COVID-19 yaani covidi virus disease 2019

MITAZAMO NA MBINU ZA KUIDHIBITI COVID-19
Kwa baadhi ya nchi za Afrika kumekuwepo na mitazamo tofauti juu ya mbinu za kukabiliana na ugonjwa huu ,zingine zikifanana na baadhi kutofautiana Leo nitajikita zaidi katika kuangalia mitazamo ya nchi yangu ya Tanzania dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 nikiigawa katika makundi mbalimbali na baada ya hapo tutaangalia mitazamo ya kila kundi mwisho nitashauri kutokana na Athari zake,

Mtazamo wa wanasiasa :
Wanasiasa hasa vyama vya upinzani awali walilipokea kwa mitazamo ya kimataifa,yaani walipokea mitazamo kutoka kwa nchi za nje hasa nchi zilizokuwa zimeshambuliwa mfano China,Afrika ya Kusini,Kenya n.k mitazamo yao ilijikita moja kwa moja kupokea na kufanyia kazi kile kinachoelekezwa na wataalamu wa afya popote duniani, wakati mwingingine watawala na mamlaka ya nchi zilizoshambuliwa na ugonjwa huu zilitoa japo baadhi ya matamko hayakuwa na positive impact mfano matamko kama rock down, wafanyie kazi na watumishi wa umma kuwa rocked down pia shule kufungwa,kuvaa maski kunawa mikono kwa sabuni ,kutumia sanitizer na kuepuka msongamano,na mbinu tofauti tofauti za kujaribu kuua au kupunguza hao virusi wasienee kama kupulizia chlorine katika majumba ,ofisini,sokoni,n.k

Mtazamo wa Serikali ya Rais Magufuli
Serikali iliyopita chini ya aliyekuwa Rais wetu hayati Magufuli ilijipambanua katika kusimamia inachokiamini na kuaminisha umma msimamo wake jambo lililopelekea wataalam wa sekta ya afya,viongozi wa kidini,wawakilishi wetu bungeni hadi mwananchi mmoja mmoja kutii na kuamini misimamo na imani juu ya ugonjwa huu na namna ya kuendeleza maisha, ilikuwa ni historia ambayo itachelewa kupotea katika masikio na macho ya wananchi na walimwengu kiujumla jinsi mitazamo ya serikali ya awamu ya tano chini ya Jemedari hayati Johni Joseph Magufuli ilivyoungwa mkono na watanzania wote cha ajabu zaidi wataalam wetu wa afya nao waliunga mkono suala la kujikinga COVID 19 kwa kupiga nyungu na kutumia dawa zetu za asili baadhi ya mataifa hayakuamini trategies zizokuwa zikitumika Tanzania dhidi ya UVICO tulionekana tofauti ila tuliendelea kuushangaza ulimwengu kutokuwa na namba yeyote ya mgonjwa wa COVID wala vifo ,baadae nchi zilizojirock down zilianza kupunguza misimamo yake hii ilitokana na nchi kuporomoka kiuchumi huku Tanzania ikiwa haijayumba sana kiuchumi jambo lililomfanya Rais wa Tanzania na watanzania kuona kama wameishinda hii vita dhidi ya COVIDI na Pengine na ugonjwa wenyewe Tanzania ilibadilisha maisha ya woga,maisha ya maski,maisha ya levelsit

Tanzania ilifungulia watalihi ,walitembelea vivutio walifundishwa kupiga nyungu n.k hii ndo serikali ya MAGUFULI
maski yaani barakoa zilivaliwa kwa hiari zaidi na kwa anayeona inafaa kwa mazingira yake

Matokeo ya msimamo na mitazamo ya serikali ya hawamu ya tano ilikuwa na athari chanya kiuchumi na ata kiafya kwa upande wa kuwaondolea hofu watanzania hilo hadi Leo limejidhihilisha kuwa mbali na njia za kiafya zinazo sisitizwa zaidi kuhusu kuzuia usambaaji wa ugonjwa huu lakini watanzania wanaonekana kuuzoea zaidi ugonjwa huu! Mfano kwenye mikusanyiko Leo mashabiki wa simba na yanga waambie wasiingie kiwanjani kuitazama dabi ya Kariakoo usikie!

Mtazamo wa serikali ya awamu ya sita
Wanasiasa wenyewe wao wanatwambia kila zama na kitabu chake ndivyo unavyoweza kusema lakini kwa upande mwingine tunaweza tukasema ni mipango ya mungu kwani kuna mambo ambayo kwa misimamo ya serikali ya awamu ya tano imeweza kuilaisishia kazi serikali ya awamu ya sita ,waswahili husema wakati ukuta sitaki kuwaupande zaidi ya kupima strategies za kila kundi na kulipambanisha na kupata suluhisho!

Serikali ya awamu ya sita mtazamo wake ni wa kitaaluma serikali ya raisi Samia SULUHU HASANI ililitazama swala la UVICO-19 kitaaluma zaidi kwa kuwapa nafasi wahusika ambapo tume iliundwa kwa kutumia wizara ya afya na kutumia wataalam wetu Madaktari baada ya kuwapa nafasi ya kufanya utafiti ambayo naweza kusema yamekuwa kama mabadiliko katika upande wa mitazamo wa awali juu ya COVID19 na matokeo yake ni

KUCHANJA CHANJO YA COVID-19 KWA HIARI
Serikali ilitangaza mtizamo mpya wa chanjo baada ya matokeo ya tafiti za wataalam maktari kabla ya apo baadhi ya wataalam walikuwa wameanza kuignore au kudhoofisha umuhimu wa nyungu yaani (kujivukiza)
Wengine walikuwa ni watendaji wakuu ndani ya serikali iliyopita jambo ambalo wananchi na baadhi ya wenzao,viongozi wa dini waliliona kama usaliti
Hii imepelekea kugawanyika kwa makundi yenye mitazamo tofauti na serikali iliyopita na mitazamo mipya ya serikali iliyopo

Mwananchi amfuate nani: Bila shaka Madaktari na wenye dhamana wizara ya afya ndio wenye kufuatwa tatizo linalochelewesha imani ni wao walishindwa kuwa na kauli moja tokea awali jambo litakalopelekea wachelewe kueleweka kwa haraka na cha msingi wasilazimishe mwananchi ila tu watoe elimu mashuleni,sehemu za ibada,mahospitalini na mitaani kwani wananchi walishazoea mazingira waliyoyatengeneza wao kwa mikono yao na kauli zao , Tatizo kinachowachelewesha ni taaluma yao waliyoshindwa kuitetea kwa wakati ule wakaingia katika mkumbo wa serikali hatimaye Leo wamerudi nyuma wameleta jambo lenye kuproof kisayansi hawakujua kuwa wakati wanatuhaminisha kwa kufanya practical sisi ambao ni wachukuaji tulilibeba tukalitumia na tushalielewa kwa imani ata pasipo.
Uthibitisho wowote kisayansi Leo ni ngumu kulikubali kwa haraka ila elimu zaidi iendelee kutolewa,mahospitalini,shuleni,na ata mitaani kuhusu umuhimu wa chanjo hii. Wanasayansi wetu wafanye utafiti wakina na baadae wakirudi kwetu wawe ni suluhisho pasipo na mash aka mwisho yoyote,

Mimi nilifundishwa kuwa kuna njia mbalia mbali za kuambukizwa magonjwa mfano

(Contangeous disease)magonjwa ya kuambukizwa kwa kugusana au mengine ya kuchangiana maji maji au damu kama Hepatitis B,HIV,n.k mfano tumeshuhudia wanaotoa huduma hiyo hawavai gloves jeikitokea ana mchbuko kwenye ngozi ya vidole au vidonda hajaambukizwa HIV au magonjwa mengine ?kama kutolewa kipimo cha malaria huvaa gloves je kwenye utafiti wenu hii ikoje ya kutovaa ?.

HITIMISHO
serikali ipate fundisho la kugawanya majukum na kuthamini taalum za RAIA wake na kuwapa nafasi,na pia wasomi wetu nikiwalenga madaktari hapa wabadilike waweze kusimamia taaluma yao bila kusukumwa na siasa au watawala mwisho naipongeza serikali kwa hatua inazochukua kushirikiana na wizara ya afya ili kujikinga au kuzuia watanzania tusiambukizane au kuambukizwa hivyo ushauri wangu kutokana na uzoefu wa ugonjwa huu kuwa mfupi watu wenye kuchanja wachanje kwa hiari na wanaoendelea na dawa na asili pamoja na nyungu waendelee

mwisho ewe msomaji mwanafamilia ,au mgeni wa jamii forum naomba nipigie kura yako*************"mungu akubariki sana.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom